Dstv Tanzania

KATIBU WA CCM MKOA WA NJOMBE NA SECTRETARIETI YA MKOA WAMESHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 19 YA MWL.NYERERE KWA KUFANAYA MATEMBEZI WILAYANI LUDEWA


Maadhimisho ya miaka 19 ya Mwl.Nyerere Wilayani ya Ludewa yaliyoongozwa na katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima wakifanya matemezi Wilayani Ludewa

Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Paza Mwamlima ameambatana na viongozi wa Secretarieti Mkoa wa Njombe ambao ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Eratso Ngole,Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Lucas Nyanda, katibu ya UVCCM Sure Mwasanguti na katibu wa UWT  Bi.Angel Milembe na wanachi mbalimbali wazalendo
Baada ya matembezi wakipata chai kabla ya kikao kuanza
Baada ya kufanya maadhimisho ya miaka 19 ya Mwl.Nyerere wamefanya kikao na viongozi wote chama kuanzia ngazi ya kata mpaka wilaya na wakuu wa idara wote toka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa.

Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe amewaomba viogzoi wa CCM wa Wilaya ya Ludewa  na wakuu wa idara wa Halmashauri ya Ludewa  kupendana  sana na kuombeana mafanikio kwani kazi wanayoifanya ni moja ambayo ni kujenga nchi na kufanya kila mtanzania awe na maisha bora.


Serikali ya awamu ya tano imeamua kuondoa umaskini wa kila kaya hivyo kila mtumishi anawajibu wa kujiuliza amekuta nini na amefanya nini katika ofisi yake.

Chama cha mapinduzi baada ya uchaguzi kiliunda serikali na serikali inataka watumishi wasifanye kazi kwa woga ila Wafanye kazi kwa tija.

Kwa ushirikiano uliopo Ludewa baina ya chama na Serikali hatashangaa kuona Ludewa inaongoza kitaifa katika nyanja zote.

CCM ni chama cha Mungu, na moja ya maajabu ya CCM ni kwamba hata kama chama hakina hela ila kila siku kinapemdeza na wanachama wake wote wanapendeza,na sasa chama kimejipanga kufanya mageuzi makubwa na kuondokana kabisa  na suala la kuomba fedha kwenye halmashauri.


Katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa aliyesimama Kulia akitoa ufafanuzi juu ya maenedeleo ya siasa kwenye wilaya yake.

Na amesema chama hakina wataalamu ila wataalamu wa Serikali ndio wataalamu wa chama na ni lazima waje watoe ujuzi wao kwenye chama.Sasa chama kimeamua kuanzia ngazi ya mashina waelewe nini chama kinafanya kwani huko ndipo wana CCM wapo wengi.

Ameomba wanaludewa wawaunge mkono viongozi viongozi waliopo madarakani  ili waweze kufanya kazi zao vizuri, kwa kufanya hivyo watakuwa wanaijenga Ludewa yao.

Sasa chama kinahakiki mali upya za chama na sio kunyang'anywa ila mali zote zitakuwa chini ya baraza la wadhamini, kuanzia sasa jumuiya zote zitakuwa chini ya chama cha mapinduzi na watumishi wote watalipwa na chama na sio jumuiya, ameomba mali za chama zilindwe kwa gharama yeyote ile ili ziwe salama.

Katika hotuba yake amesema ardhi ndio huzaa kila kitu. Kwani ardhi ni moja ila hutofautiani kwa fulsa, amewaomba wataalamu walisomea  mambo ya kilimo  wasaidie kujua fulsa gani zinafaa katika ardhi iliyopo.

Pia amewaomba wananchi wa Ludewa kumtumia Mkuu wa Wilaya kwa kasi kwani ni mtu anayependa maendeleo na anaunganisha chama na serikali kwa nguvu zote.

Katibu wa CCM mkoa amemwomba katibu wa CCM Wilaya ya Ludewa kufanya ziara za kutosha kuanzia ngazi ya shina ili kupata wanachama wengi, uzuri wa Wilaya huwa haudumu    milele hivyo amewaomba wanaludewa kuutumia uzuri huo wa Ludewa kujenga chama na Serikali. 


Katibu wa CCM Mkoa ameomba  vijana wajenge chama na serikali na vijana watumike katika shughuri zote za ujenzi wa serikali na chama kwani ndio nguvu kazi ya Taifa letu.

"Mwana CCM yeyote halalamiki na ukiona analalamika huyo si mwana CCM" Mwamlima amesema.  


Aidha amesema chama kinabadilisha kadi za uanachama na kwenda kutumia kadi za electronic, kadi hiyo otakuwa na taarifa zote za mwanachama

Na mwisho amesema anaondoka Ludewa akiamini amekuja kwenye mkoa bora.
Wakiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh.Tsere


Wakiaga na kuanza Safari ya kurudi Mkoani Njombe

 wamepata fulsa ya kufika shule ya Secondary Madunda


Na Erasto Kidzumbe
0753580894












Hakuna maoni: