Dstv Tanzania

KATIBU WA VIJANA WILAYA YA LUDEWA ASHIRIKIANA NA CHIPUKIZI KUADHIMISHA KILELE CHA MIAKA 19 YA MWL.NYERERE KWA KUFANYA USAFI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA

Pichani aliyeshika vifaa vya kufanyia usafi ni katibu wa UVCCM (W) Ludewa Hassan Kapolo

Katibu wa Vijana wa Ludewa akishirikiana na chipukizi wameadhimisha kilele cha miaka 19 ya kifo cha Mwl.Nyerere kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Ludewa, wakiongozwa na katibu wa vijana wa CCM Wilaya ya Ludewa Hassan Kapolo.

Chipukizi wameadhimisha Kilele hicho huku wakiungwa mkono na vijana wengi wa CCM na vijana wengine wazalendo wa taifa la Tanzania, chipukizi wamemshukuru katibu Kapolo kwa kuwaunganisha na kufanya chipukizi waanze kuziishi fikra za Mwl.

Katika maadhimisho hayo katibu wa Vijana amewaomba chipukizi wafanye kazi kama kauli mbinu ya mwalimu inayosema "Utu wa mtu hupimwa kwa kazi"

Na Erasto Kidzumbe
0753580894


Hakuna maoni: