Dstv Tanzania

VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE NA WILAYA YA NJOMBE WASHIRIKI MAZISHI YA JOHN MWANDOLOMA DIWANI MSTAAFU WA KATA YA KITANDILILO MAKAMBAKO


Pichani ni viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe wakiwa katika maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Diwani Mstaafu  John Mwandoloma wa kata ya Kitandililo Makambako

Viongozi wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Njombe wamepokea kwa masikitiko makubwa juu ya msiba huo kutokana na mchango mkubwa aliokuwa nao John Mwandoloma katika chama.

Hata hivyo jopu kubwa la viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Njombe washiriki mazishi ya aliyekuwa Diwani mstaafu

Katika mazishi hayo viongozi wa CCM wametoa rambirambi mbalimbali na nasaha mbalimbali  ikiwa ni pamoja  na kuwataka wananchi na watanzania kwa ujumla kujiweka tayari wakati wote kwani hapa duniani tunapita tu.

Sio hivyo tu, mwisho wameomba wananchi wote kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kumudu kasi ya mheshimiwa Rais, usipo fanya kazi kwa bidii utaona kila kitu hakiendi na mwisho utaishia kutoa lawama zisizokuwa na sababu yeyote.

Na Erasto Kidzumbe
0753580894






Hakuna maoni: