KATIBU WA UWT MKOA WA DAR ES SALAAM GRACE HAULE ALIYEKUWA KATIBU WA UWT WILAYA YA NJOMBE AFANYIWA HAFLA FUPI YA KUAGWA NJOMBE
Pichani ni katibu wa UWT Mkoa wa Dar Es Salaam Bi.Grace Haule, aliyekuwa katibu wa UWT Wilaya ya Njombe
UWT Wilaya ya Njombe wamefanya hafla fupi ya kumwaga Bi Grace Haule Katibu wa UWT Mkoa wa Dar Es Salaam aliyekuwa Katibu wa UWT Wilaya Njombe.
Hafla hiyo imehudhuriwa na watumishi mbalimbali wa Chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka Wilaya,Mjumbe wa mkutano mkuu taifa, MNEC, pia imehusisha baadhi ya wabunge wa viti maalumu Dkt.Suzan Kolimba na Neema Mgaya na wajumbe wa baraza UWT Mkoa wa Njombe.
Mwenyekiti wa UWT amesema wanafanya haya kwasababu alikuwa ni kiongozi aliyejua misingi ya kazi na kufanya jumuiya ya wanawake ikimbie kwa muda mfupi aliofanya kazi katika Wilaya ya Njombe, jumuiya imefanya mambo makubwa kwa kipindi kifupi sana
Kupitia utumishi wake hawana sababu ya kutokumuaga kwa heshima japo wanajua ameacha pengo kubwa katika Wilaya ya Njombe "Bi. Angel Mwangeni amesema hayo"
UWT Wilaya ya Njombe wamemuandalia zawadi nyingi ikiwa ni ni ishara tosha kuwa alikuwa kiongozi aliyewafaa wakati wa shida na raha
Katibu wa UWT Mkoa wa DSM akipokea zawadi mbalimbali
Katika hafla fupi Dkt.Suzan Kolimba anampongeza sana kwa kazi kubwa anayoifanya Bi. Grace Haule, kwani kwa muda mfupi huu aliokaa pale DSM ameshapokea sifa nyingi juu ya utendaji kazi wake. Hata hivyo wenyeji wake wa DSM wanasema UWT Wilaya ya Njombe wamefaidi sana uwepo wa katibu huyu na sasa ni zamu ya UWT DSM. Dkt. amempa zawadi ya TSHs,200,000/= kwa ajiri ya kufanya maandalizi anapo anza maisha mapya.
Pia Mkurugenzi wa Shule ya Living Stone ambaye ni diwani mstaafu amepata kusema haya katika salamu zake "tumekuwa tukipokea viongozi wengi katika ngazi za Mkoa na Wilaya lakini wakiwa wanaondoka hatuwajali, lakini UWT Wilaya ya Njombe mmefanya jamabo kubwa na ameomba liwe jambo endelevu kwenye Jumuiya zote na Chama kwa ujula"
Katibu akishukuru kwa ajili ya Shukrani na ushauri alioutoa Luvanda
Katika salamu, mwisho katibu wa siasa na Unezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole, amesema anasikitika sana juu ya kuondoka kwa Grace Haule, maana alikuwa ni kiongozi mwanamke wa pekee asiyekata tamaa na siyekatishwa tamaa kwa watu wengine, alikuwa mvumilivu.
Mwisho mwenezi ameomba pamoja na sifa zote wanazompa watu, lakini aendelee na moyo wa kupenda kazi na kujishusha kwani furaha ya mwenezi ni kuona katibu anafanikiwa zaidi na sio kuharibikiwa.
Mwisho katibu wa siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe amempa zawadi wa fedha TSHs 200,000/= kwa ajili ya kwenda kuanzia maisha, lakini mwenezi amempongeza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe, Rosemary Lwiva kwa kumpa fedha kiasi cha TSHs 50,000/= kwani ndio kiongozi aliyemuandaa Grace na kufanya aonekane na kuwa mtu wa pekee na mwisho amemzawadia Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Bi.Angel Mwangeni fedha kiasi cha TSHs 40,000/=kwani waliishi vizuri,kufanya kazi vizuri na kumsemea vizuri mbele za watu.
Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akimkabidhi zawadi ya fedha kwa katibu wa UWT Mkoa wa DSM Bi.Grace haule
Kabla ya kufunga sherehe Luvanda ambaye ni diwani mstaafu amemfanyia sara ya kumkabidhi mikononi mwa Mungu kwa ajili ya kwenda kufanya kazi kwa kumtegemea Mungu.
Kwani uongozi si kazi rahisi kama tunavyofikili kwa nguvu za kibinadamu ni ngumu sana kufanikiwa zaidi ya kujikabidhi kwa Mungu
Katibu wa UWT Mkoa wa DSM akifanyiwa sara kwa ajiri ya kumkabidhi kwa Mungu juu ya kazi kubwa anayoenda kufanya DSM
Na mwisho katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagie amesema anamtakia kazi njema, ila popote atakapokutana na ugumu asisite kumpigia simu na kuuliza. Hata hivyo katibu wa CCM amesema DSM kuna wazee wengi na waasisi wa chama cha mapinduzi wapo pale, amemwomba Bi.Grace awe mtu wa kujifunza mazingira kwa haraka ili aweze kufanya kazi kwa urahisi.
Pichani aliyesimama ni Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike akimwaga Katibu wa UWT Mkoa wa Dar Es Salaam
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni