Dstv Tanzania

KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE AMEAMBATANA NA KATIBU WA UVCCM MKOA WA NJOMBE SURE MWASANGUTI KUZUNGUMZA NA BAADHI YA WANAFUNZI WA CHUO CHA AMANI NJOMBE.


 KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE ERASTO NGOLE AMEAMBATANA NA KATIBU WA UVCCM MKOA WA NJOMBE SURE MWASANGUTI KUZUNGUMZA NA BAADHI YA WANAFUNZI WA CHUO CHA AMANI NJOMBE

Viongozi hao wamepata fulsa ya kuzungumza na wanafunzi mambo mengi ambayo yanaweza kuwasaidia ili waweze kufanikiwa.

 Namna ya kutumia fulsa nyingi zilizopo Mkoa wa Njombe ili kuweza kufanikiwa katika malengo yao wanayojiwekea pindi wakiwa masomoni na hata baada ya kumaliza masomo yao.

Katika mazungumzo hayo Erasto Ngole amesema jambo la kwanza ili uweze kufanikiwa usiwe mtu wa kukata tamaa kwani hao wote unaowaona wamefanikiwa, jua wameumia kwa muda mrefu na wamekuwa wavumilivu kwa mambo mengi. Ndio maana wameweza kufanikiwa.
Pia amewaomba vijana kuwa wazalendo na nchi yao, kuipenda nchi na kuitunza na kuhakikisha kwa namna yeyote nchi hii inakuwa salama.

Hata hivyo amewaomba wazuoni hao kuwa na malengo ya muda mrefu na muda mfupi ili kuweza kupima kama malengo hayo yanafanikiwa au hayafanikiwi, hii inamaana ukiwa huna malengo huwezi jua kama unafanikiwa au hufanikiwi.

Licha ya hayo yote amewaasa wanafunzi kuwa mafanikio sio shule tu, ila kuna mambo mengi yanayoweza kichangia mtu afanikiwe.
Akiwaasa wanafunzi hao amewambia ni vizuri kwa vijana kushiriki shughuri za kijamii ili kuweza kujua nini kinaendelea katika jamii zetu zinazo tuzunguka.

Mwisho amewaomba wanafunzi kutumia fulsa zote zilizopo na zinazojitokeza katika jamii zetu, hii itasaidia vijana kujipatia kipato na kufanya maisha yaendelee.

Pamoja na hayo,  wanafunzi wameomba “Printer”  yenye thamani ya THs 800,000/=, ikiwa ni moja ya mtaji katika kuendesha shughuri zao za mradi wao,  katibu wa siasa na uenezi amesema kwa kuwa wameomba kwa mzazi, na uwezo wa kuwasaidia anao, amekubali ombi lao na kuwanunulia  printer hiyo.

Hakuna maoni: