MBUNE VITI MAALUMU NEEMA MGAYA ASHUSHA NEEMA WILAYA YA LUDEWA
Mh.Mbunge viti maalumu Neema Mgaya akimfunika mgojwa
Mbunge wa viti maalumu wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa
Njombe Neema Mgaya,ametoa msaada wa mashuka ya kulalia wagonjwa pamoja
na mifuko ya saruji kwa ajili ya kuchangia nguvu za wananchi katika
ujenzi wa zahanati na vituo vya afya katika wilaya ya Ludewa.
Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo katika kituo cha
afya Ludewa ‘’K’’,Lugalawa, Mlangali pamoja hospitali ya wilaya hiyo
Mbunge Neema amesema ametoa misaada hiyo kutokana na kwamba serikali
kupitia chama cha mapinduzi CCM imejizatiti kuhakikisha inaboresha
huduma za afya kwa kila kijiji zahanati kila kata kituo cha afya.
‘’Nimetoa mashuka zaidi ya 60 kwa wilaya hii pamoja na
saruji zaidi ya tani mbili ni hii yote ni kutokana na uhitaji uliopo na
nitafika kila wilaya katika mkoa huu…mifuko hii ya saruji inakwenda
kuunga mkono juhudi za wananchi wetu..nipo hapa kwa ajili ya kutekeleza
ilani ya chama cha mapinduzi CCM’’amesema Neema Mgaya.
Akizungumza mara ya kupokea msaada huo mmoja wa wakazi wa
Lugarawa Firomenda Haule amesema wanamshukuru mbunge huyo kwa kuunga
mkono juhudi zao na kwamba wanaamini changamoto zao nyingine
zitafikishwa bungeni.
‘’Tunamshukuru Mbunge Neema kwa kutuunga mkono na kwamba
kama mbunge mwanamke utaendelea kufikisha changamoto zetu nyingine za
kuanzisha ujenzi wa vituo vya afya’’amesema Firomenda.
Pia Mbunge huyo akiwa katika ziara yake hospitali ya wilaya
ya Ludewa mganga mkuu wa hospital hiyo dkt Nelson Kimolo,alimueleza
Mbunge huyo kuwa wanakabiliwa na upungufu wa madaktari akiwemo mtaalamu
wa usingizi katika wodi ya upasuaji hali inayokwamisha wakazi wa wilaya
hiyo kupata huduma ya upasuaji hospitalini hapo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni