Dstv Tanzania

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) CHAWAUNGA MKONO UMOJA WA WANAWAKE WA TANZANIA (UWT) KWA KUFANYA KONGAMANO KUBWA LA KUMPONGEZA NDG. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI


17 Novemba 2018

Katika Kongamano kubwa la kihistoria la Kumpongeza Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM ambalo limeandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi kwa niaba ya CCM amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawaunga mkono na kuwapongeza UWT kwa kuandaa Kongamano hilo la kubwa  kihistoria.

Akiwasilisha salamu za CCM katika Kongamano hilo  Ndg. Polepole amsema Rais Magufuli amefanya mengi ndani ya Miaka mitatu yanayonufaisha wanawake ikiwemo ujenzi na ukarabati wa zahanati na vituo vya afya vingi, ujenzi na ukarabati wa miradi mikubwa ya Maji safi na salama, utetezi wa maslahi ya wakulima ambao wanufaika wengi ni wanawake, kuondoa riba kwenye mikopo inayotolewa na Serikali kupitia  Halmashauri zote nchini na kuwazingatia wanawake sana katika nafasi mbalimbali za uongozi wa kuchaguliwa na wakuteuliwa, hivyo wanawake wa Tanzania wanakila sababu ya Kumpongeza, Kumuunga mkono na kumuombea Rais Magufuli katika utumishi wake kwa Watanzania.

Aidha Ndg. Polepole amepokea Tuzo ya Pongezi kwa niaba ya Ndg. Magufuli  kutoka kwa Uongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Kongamano hilo ambalo limefanyika Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Temeke Ukumbi wa Sabasaba limehudhuriwa na Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Maelfu ya Wanawake kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania wakiongozwa  na Ndg.
Gaudensia Mugosi Kabaka Mwenyekiti wa UWT Taifa.

Imetolewa na

*IDARA YA ITIKADI NA UENEZI*
*CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)*

Hakuna maoni: