Dstv Tanzania

MKUU WA WILAYA YA KILINDI MH.SAUDA MTONDOO AKUTANA NA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO NA KUTEMBELEA MRADI WA REA.

PICHANI:Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo akiongea baadhi ya wataalamu wa REA katika kijiji cha Makasini.

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mh Sauda Mtondoo ameongozana na Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Makasini kupita kwa wafanya Biashara ndogo ndogo eneo la Kwediboma kwa  lengo kusikiliza kero zao na kuzitolea ufumbuzi.
PICHANI:Baadhi ya wafanya biashara wadogowadogo  wa kijiji cha Makasini katika eneo la kwediboma wakiongea na Mh. Mkuu wa Wilaya

Lakini pia Sambamba na Kusikiliza Kero za Wafanya Biashara ndogo ndogo Mh Mkuu wa Wilaya aliweza kukagua mradi wa Umeme wa REA uliopo Kijiji cha Gombero Katika Kuhakikisha Maagizo ya Waziri wa Nishati Mh. Merdad Kalemani yametekelezwa tangu alipofanya ziara wilayani humo mnamo tarehe 8/10/2018.Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kilindi aliongozana na Katibu Tawala wa Kilindi ,Kaimu Meneja Tanesco Wilaya ya Kilindi pamoja na Viongozi wa Kijiji Cha Gombero

@Kilindiyetu

Hakuna maoni: