KATIBU WA CCM WILAYA YA NJOMBE ANTHONY KATANI ATEMBELEA KAMBI LA VIJANA WA UVCCM MKOA WA NJOMBE LINALOFANYIKA ULEMBWE SEKONDARI
PICHANI:Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Ndg,Anthony Katani akizungumza vijana wa UVCCM Mkoa wa Njombe walioshiriki kambi la kutengeneza "Block" kwa ajili ya kujenga Hosteli ya wasichana Shule ya Sekondari Ulembwe.
Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Anthony Katani ametembelea kambi la umoja wa Vijana Mkoa wa Njombe, linalofanyika Ulembwe Sekondari kwa ajili ya kutengeneza "block" za kujengea Hosteli ya wasichana katika Shule ya Sekondari Ulembwe.
Katibu amefurahishwa na jitihada zinazofanya wa Bodi ya shule ili kuweza kunusulu watoto wa kike kupata mimba za utotoni, utoro uliokithiri na kushuka kitaaluma. Kwani kwa kujenga Hosteli hizo yawezekana kuwa ndio moarobaini wa matatizo hayo yanayowakabili watoto wa kike.
Hata hivyo katibu amewapongeza vijana wa UVCCM walioshiriki kambi hilo la uzalishaji kwani kazi nyingi za chama nizakujitolea hivyo popote watakapohotajika amewaomba wakafanye kazi hizo kwa kujitolea na kwa bidii kwani vijana ndio nguvu kazi inayotegemewa katika Taifa letu.
PICHANI: Kushoto ni katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Anthony Katani, akifuatia katibu wa UWT Wilaya ya Njombe Nuru mwaibako ,akifuatia Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe Jocktan Mtewele na Mwisho ni mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve wakifanya mazungumzo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Nebchard Msigwa amesema anaamini hakuna namana nyingine ya kumpongeza Mh. Rais zaidi ya kufanya kazi kwa bidii.
Mwenyekiti wa bodi shule ya Sekondali ulembwe aliyesimama kushoto Nebchard Msigwa akiwashukuru viongozi wa CCM Wilaya ya Njombe na Mkoa wa Njombe kwa kupeleka chakula kwa ajili ya vijana wa UVCCM wanaoendela na kambi.
Na Erasto Kidzumbe
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni