Dstv Tanzania

JOHNSON ELLY MGIMBA KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI MKOA WA NJOMBE AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA VIBANDA VYA CCM NA UKUMBI TAWI LA ILININDA.


PICHANI:Katibu wa hamasa na chipukizi Mkoa wa Njombe Johnson Mgimba akiongoza harambee ya kujenga vibanda vya CCM tawi la Ilininda.

WanaCCM tawi la Ilininda Kata ya Madilu Wilayani Ludewa Jana tarehe 16.12.2018 kulikuwa na harambee ya Ujenzi wa Vibanda vya Biashara na Ukumbi Mali ya Tawi hilo.

Katika Harambee hiyo Mgeni Rasmi alikuwa *Ndugu Johnson Elly Mgimba* Katibu wa Hamasa na Chipukizi Mkoa Njombe.

Ambapo awali mwenyekiti wa Tawi akisoma taarifa na Risala kwa Mgeni Rasmi ilionesha wao kama Tawi walikuwa wamejipanga na walikuwa wanaomba msaada wa kujenga vibanda vya Mabanzi ambavyo bajeti yake ilikuwa 1,200,000/= na ni vya  muda mfupi lakini Mgeni Rasmi aliwabadilisha palepale kwakuwaomba waondokane na mawazo ya kujenga vibanda vya mabanzi.

Eneo lao lipo Mjini kabisa hivyo akawaomba wajipange vijengwe vibanda vya Tofali na vya kisasa kabisa na kisha akawaongezea kuwa Ilininda pana uhaba wa Ukumbi wa sherehe hivyo akawaambia nyuma ya vibanda hivi kujengwe Ukumbi mkubwa utakaotosha kwa shughulu za kijamii zinazofanyika kijijini hapo.

Hapo ndipo Sura ya Harambee ilipobadilika na watu kuanza kuchangia kwakuzingatia mapendekezo ya Mgeni Rasmi ambapo waliyapokea na kuyakubalia.

Hivyo Michango yote iliyotolewa kwa jumla ya ahadi na Taslimu ilikuwa kama Ifuatavyo;
1.Fedha Tsh.450,100
2.Tofali   9,650
3.Mifuko ya Cement 29
3.Bati  20
4.Mbao lati  100
5.Fremi 1.
6.Gharama za kutengeza fremu zote zilizobaki zipelekwe mbao tuu.
7.Kada Moja amejitolea Ufundi wa kujenga bure yeye kazi ikianza.

*Jumla ya Vitu vyote vilivyopatikana  vikithaminishwa kwenye Fedha ni Tsh.2,600,000/=*

Mwisho Mgeni Rasmi aliwashukuru kwa mwitikio na aliwapongeza viongozi wake wa  Tawi kwa ubunifu huo na akawahakikishia kuwa Chama kwa sasa kimerudi kwa wanachama hakuna wanaomiliki chama kwa sasa zaidi ya wanachama.

Pia aliwasisitiza kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani kuhakikisha kijijini hapo wanatetea nafasi zote za wenyeviti wa vitongoji na kisha Mwenyekiti wa Kijiji.

Katibu Kata wa Kata ya Madilu pamoja na Mwenezi wa Kata wote walitoa pongezi kwa Tawi hili Kuja na ubunifu  huo. Lakini katibu Kata amemsifu Mgeni Rasmi kwa moyo wake wa uzalendo kwa chama chake na akasema anamkumbuka na atamkumbuka kwa mambo mengi anayofanya kwa jamii yake.

Ahsante.

Hakuna maoni: