MAKAMU MWENYEKITI CCM (BARA) NDG. PHILIP MANGULA ATOA PONGEZI KWA MBUNGE WA JIMBO LA WANGING'OMBE ENG.GERSON LWENGE
PICHANI:Makamu mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg.Philip Mangula
Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania bara Ndg.Philip Mangula amempongeza Mbunge wa Jimbo la wanging'ombe Eng.Gerson Lwenge kwa utaratibu alioweka wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kila mwaka.
Amempongeza Mbunge huyo katika kikao cha kusoma utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka mitatu mfululizo, hata hivyo amemshukuru Mbunge lwenge kwa namna ya utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Ilani CCM.
Makamu Mwenyekiti ameomba viongozi wa chama kuongeza bidii ya kufanya ziara za chama na jumuiya ili kuwafikia watanzania wote hadi kwenye mashina kwani watanzania wanataka kujua serikali imefanya nini tangu mwaka 2015.
Katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Ndg. Erasto Ngole amemwomba katibu wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe na wilaya nyingine zinazounda Mkoa wa Njombe kuongeza bidii ya usajili wa wanachana kwa njia ya kieletronic. Akiwa anawaomba waongeze bidii amesema ifikipo tarehe 5/2/2019 kwa kiwango cha chini kila Wilaya iwe imesajili wanachama elfu tatu(3000)
Katibu wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Njombe Ndg. Lucas Nyanda akimwakilisha katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg. Paza Mwamlima, amewaomba viongozi wote wa chama na Serikali kuuishishi umoja na Mshikamano katika shughuli za kila siku za utumishi.
Mbunge Eng.Gerson Lwenge katika taarifa yake ya utekelezaji ametoa pikipiki mbili zenye gharama ya shilingi Milioni nne laki mbili na elfu hamsini(4,250,000/=)kwa umoja wa vijana ikiwa ni moja ya mradi wa kuwaingizi fedha. Hata hivyo ametoa fedha kwa ajili ya kutengeneza mashine ya kukamua mafuta ya alizeti kwa Umoja wa Wanawake ikiwa ni mradi wa umoja wa wanawake.
Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe
Maoni 1 :
Hongera sana Mh.Lwenge Mbunge wetu kwa kazi nzuri,Mungu akubariki.
Chapisha Maoni