VIONGOZI WA CCM TAIFA WAUNGANA NA WANANJOMBE KUTOA POLE KWA WAFIWA WA WATOTO
Katibu wa uchumi na fedha wa CCM Taifa Dr.Frenk Hawasi Haule akitoa salamu kwa viongozi wa CCM (M) Njombe
Viongozi CCM Taifa wameungana na wana CCM Mkoa wa Njombe kulaani vikali mauaji ya watoto yaliyotokea ndani ya miezi minne yanayohusu watoto kutekwa na kuuwawa kikatili ndani ya Mkoa wa Njombe. Matukio hayo yanachafua taswira ya mkoa wa Njombe na Taifa kwa ujumla.
Viongozi hao wa CCM ngazi ya Taifa ambao ni katibu wa uchumi na fedha wa CCM Taifa Dr.Frenk Hawasi Haule,
katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanal Mstaafu Ngemela Lubinga na katibu wa Umoja wa UVCCM taifa Mwl.Raymond Mwangwala
Mlezi wa Mkoa wa Njombe Dr.Frenk Hawasi Haule amewaeleza viongozi wa CCM (M) wa Njombe kuwa viongozi wa ngazi ya taifa wanalaani mauaji haya kwa ni jambo la kusikitisha na lisilokubalika, Njombe ni Mkoa wa wa amani na utulivu. Tumeielekeza serikali watu wanaohusika na mauaji haya watafutwe na wachukuliwe hatua za kisheria na tumaamini watu hawa watapatikana.
Kanal Mstaafu Ngemela Lubinga Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akizungumza na viongozi wa CCM (M) Njombe
Kanal Mstaafu Ngemela Lubinga, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, amesema Mkoa wetu wa Njombe ni Mkoa wa amani na utulivu, hata hivyo wazazi waliopteza watoto hawa ni watanzania wenzetu hivyo ni lazima tuwe tayari kutoa ushirikiano katika vyombo vya dola ili kuweza kubaini watu wanao husika na matukio haya.
Katibu mkuu umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mwalimu Raymund Mwangwala amesema kuwa mauaji ya watoto wadogo mkoani Njombe ni moja ya eneo lililogusa umoja wa vijana kwakuwa waliofariki ni sehemu yake anayoingoza hivyo amesikishwa sana na matukio hayo ya mauaji.
Kama sisi sote ni wazalendo wa nchi yetu, linapotokea jambo kama hili huzuni ni vizuri kuungana pamoja na kuweza kutafuta ufumbuzi sio kuchukua tukio kama hili na kuweka la kisiasa huu sio usazalendo ila ni siasa za maji taka zisizo na taji katika taifa letu.
Kidzumbe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni