MNEC THERESIA MTEWELE AMEWAOMBA WAHITIMU WASIWE MZIGO PINDI WANAPOHITIMU MASOMO YAO.
PICHANI:MNEC Theresia Mtewele akiongea na wanazuoni katika mahafari ya kwanza Idara ya vyuo vikuu Mkoani Njombe
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bi. Theresia Mtewele amewataka wanafunzi wanaohitimu masomo wasiwe mzigo katika jamii, ameeleza kuwa elimu waliyopata wakiwa vyuoni isaidie kutatuta changamoto katika jamii.
Ameyasema hayo katika mahafari ya kwanza ya Idara ya vyuo vikuu Mkoa Njombe, MNEC amewoamba Vijana pindi wanapomaliza masomo na kurudi nyumbani wakatumie elimu wanazozipata vyuoni kujiimalisha kiuchumi na sio kuwa mzigo kwa wazazi na kuwa vijana wa kulalamika kila kukicha.
Amesema Serikali ya haiwezi kuajili wahitimu
wote wa vyuo vikuu, ajira hizo hazipo hivyo wanapaswa kufikili zaidi kujiajili
na sio kuajiliwa.
“Watu wengi wanaojua fulsa ni wale
ambao hawajamaliza hata darasa la saba hivyo elimu mlizopata zisiwafanye mchague kazi”
“Asiyefanya kazi na asile, Hapa kazi tu na
Tukutane kazini”
Kwa kijana aliyetulia kabisa na anafiriki vizuri
anaweza kupata kitu cha tofauti kwenye kauli mbiu hizi’’ MNEC amesema.
Njombe ni Mkoa wa fulsa kwani fulsa
nyingi zipo Mkoa wa Njombe, tatizo vijana wengi hawataki kujishughulisha na
hawapendi kutumia ujuzi wao kwa maslahi ya jamii.
PICHANI:Wanafunzi zaidi ya mia moja wakila kiapo baada ya kujiungana na CCM
MNEC akimtunuki cheti cha uanachama wa CCM moja ya mwanafunzi aliyehitimu masomo yake.
Nafarijika sana ninapo ona vijana wengi wanajiunga na CCM kwani vijana hawa wamejua mchango wa chama cha Mapinduzi katika taifa hili, Antony Katani Katibu wa CCM Wilaya Njombe amesema.
PICHANI:Wanafunzi zaidi ya mia moja wakila kiapo baada ya kujiungana na CCM
Nafarijika sana ninapo ona vijana wengi wanajiunga na CCM kwani vijana hawa wamejua mchango wa chama cha Mapinduzi katika taifa hili, Antony Katani Katibu wa CCM Wilaya Njombe amesema.
Mbunge
wa Njombe Mjini Edward Mwalongo amewaomba vijana kuwa wanachama wa CCM na sio
kuwa wanasiasa kwani siasa ni imani.
Ukiwa
mwanachama wa CCM lazima uwe tayari kujitolea ili chama cha mapinduzi kiweze
kujiimalisha zaidi na zaidi.
Kila aliyehitimu katika mahafari hii ya kwanza anapoondoka ahakikishe anaondoka na cheti cha safari au barua ya utambulisho na akaripoti ofisi za CCM za wilaya au Mkoa ili ukaendelee kufanya kazi za CCM, ameyasema haya Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve alinapowasalimia wanazuoni.
Imetolewa na Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe.
0753580894
Kila aliyehitimu katika mahafari hii ya kwanza anapoondoka ahakikishe anaondoka na cheti cha safari au barua ya utambulisho na akaripoti ofisi za CCM za wilaya au Mkoa ili ukaendelee kufanya kazi za CCM, ameyasema haya Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve alinapowasalimia wanazuoni.
Picha ya Pamoja baada ya kumaliza mazungumzo na wanazuoni Mkoani Njombe.
0753580894
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni