KATIBU HAMASA NA CHIPUKIZI WILAYA YA NJOMBE AUAGA UKAPERA
HII NI HABARI KUBWA ILIYOTIKISA HALMASHAURI
TATU ZA WILAYA YA NJOMBE.
Licha ya umaarufu wake wa kisiasa
aliyojizolea mkoani Njombe ,wa kusisimua jukwaa kwa misemo au kuiga nukuu za
mwalimu nyerere Ndugu Iman Mahmoud Moyo, lakini bado alikuwa anamiliki kadi ya
mabachala au makapera.
Uaminifu aliouonyesha katika
kukitumikia chama hicho hivi karibuni ameokana kufanya usaliti mkubwa kwa chama
hicho pale alipoamua kushuka jukwaani na kuuaga rasmi ukapera kwa kuvuta jiko
kutoka pande za ardhi yenye hadhi la jiji Dodoma.
Ndoa hiyo iliyofungwa kwa dini ya
kiislamu mkoani Njombe,ni bahati kubwa na baraka tele Dodoma limekuwa jiji hivi
karibuni na kumzawadia zawadi ya pekee nguli huyo wa siasa kupata msaidizi wake
wa karibu(shemeji yetu).
Ni muda tu ulikuwa unasubiriwa pale
Wazee Wa mji waliokabidhiwa shughuli hiyo ,Licha ya taratibu za kidini Lakini
mipango mikubwa na hekaheka ilionekana kuongozwa vyema na mzee mwenye busara
mjini hapa na mkongwe wa siasa ,mwenye jukumu la kulea vijana anayeimudu vyema
jumuiya yake kwa nafasi ya utendaji mkoa Ndugu LUCAS NYANDA (Katibu wa Jumuiya
ya Wazazi mkoa),akiwa na wasaidizi wake wa karibu.
Viongozi hao walioonekana kumudu
kila idara Afisa wa jumuiya ya vijana ngazi ya mkoa Ndugu Chone na katibu wa
wilaya ya Njombe Ndugu Daniel muhaza.
Hapa kuwa na shaka kwani jambo hilo
la kuoa lilikamilika vyema kwa kudra za mwenyezi Mungu ,watoto wa mjini
wanasema Deal Done.
Kuoa ni jambo jema na la busara tena
la heshima hivyo wadau ,rafiki ,wanachama wa ccm na Ndugu kwa sauti moja ni
pongezi kubwa kwako comrade Iman moyo kwani tunaamini Mwenyezi Mungu
atawaongoza vyema kuwa na maisha mema na yenye baraka.
Chama cha mabachala na mapakapera
umetuachia pengo lakini tunatoa pongezi kwa maamuzi sahihi na kwa muda mwafaka
tunakutakia kila lakheri katika maisha ya Ndoa hiyo .
Shukrani za dhati kwa wote
waliofanikisha kufungwa kwa Ndoa hiyo.
Licha ya taratibu zote kukamilika
sherehe kubwa inatarajia kufanyika Jumapili tarehe 01/07/2018, Mtaa wa matajiri
wa Mjini Nazarethi ,Hivyo wadau wa karibu wa kiongozi huyo tunakaribishwa
kumkaribisha shemeji yetu rasmi.
Ahsanteni mletaji wenu hapa
.......stambuli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni