Dstv Tanzania

KATIBU UVCCM MKOA WA NJOMBE AWASIFU WALIMU NJOMBE KATIKA KUTAMBUA MCHANGO WA CCM KATIKA KUWAJALI WALIMU.


"Uongozi ni utumishi na sio utukufu " 

Hayo ndio mambo yanayopatikana ndani ya mkoa wa Njombe ,Ukiachana na vivutio vya utalii kule Nyumbanitu, ambapo kila jumuiya ya ccm ilivyosimama imara katika kuhakikisha inatetea wanyonge ndani ya mkoa wa Njombe.Kwa sasa ccm mkoa wa Njombe imekuwa ikipambana kuhakikisha maslahi ya kila mwananchi yanapatikana kwa wakati na kila mmoja kuhakikisha anafaidi keki ya taifa letu bila kubugudhiwa.

Ni yuleyule katibu wa uvccm mkoa wa Njombe Comrade Sure I Mwasanguti amezidi kuchanja mbuga na viatu vilevile vyenye baraka kutoka kwenye ardhi yenye hadhi la jiji ,kwa kuonyesha uwezo wake wa kujenga mahusiano mazuri na yenye tija kwa wafanyakazi wa serikali na sekta binafsi,Mahusiano yameonyesha matokeo chanya pale usuluhishi unavyofanikiwa katika kutatua changamoto baina ya mwajiri na mwajiriwa kupitia jumuiya yake kwa kushirikiana na ccm.

Walimu mkoani Njombe wameonekana kuwa jiran na Gwiji wa siasa huyo asiyeishiwa mipango kuhakikisha mambo yanakaa sawa ,pale alipowatulita walimu walipokuwa wakitafuta haki yao pale walipopata uhamisho kutoka sekondari na kwenda shule za msingi hivyo ccm kulazimika kutafuta suluhu na kuhakikisha maslahi ya walimu hao yanapatikana.

Katibu uvccm ameonekana kuwapongeza walimu kwa kuwekeza imani yao kwa ccm ,kwani wameamini ccm inaweza kuwatatulia changamoto zao.

Mwasanguti amewaomba kuendelea kuwekeza imani zaidi kwao kwani kazi kubwa wao ni kuhakikisha mambo yanakwenda sawa kwa wapiga kura wao.

Aidha comrade mwasanguti ameonekana kupiga hatua zaidi kwa kuwapa imani zaidi walimu hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri wa ccm kwani ccm imejipanga kuhakikisha wote wenye changamoto zinatatuliwa na kuhakikisha kila mmoja inakuwa na amani,amewaomba pia waajiri na wao kuhakikisha wanajari maslahi ya watumishi wao kwani ili mfanyakazi afurahie kazi yake ni lazima apate haki zake za msingi.wao kama ccm hawatakuwa tayari kumfumbia macho mwajiri yoyote ambaye hatajari maslahi ya wafanyakazi wake kwani kazi kubwa ni kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ,kwani mwajiri wa wote ni ccm na ndio wenye dhamana ya watumishi kwani wamewaamini wasaidie kutekeleza ilani ya ccm na wanawajibu kwani taifa limetumia gharama nyingi kuwasomesha na hivyo ni lazima wahakikishe elimu zao zinatumika kulisaidia taifa letu.

Wao kama ccm ili mfanyakazi afanye kazi vizuri ni lazima awe kwenye mazingira tulivu na salama yenye kumjengea uwezo wa kufanya kazi na kama kunamabadiliko basi taratibu zote za kisheria zifuatwe hawanasababu ya kukurupuka na kuburuzana wakati mambo yote yameainishwa katika taratibu za ajira.

Pia amemsifu mwenyekiti wake Ndugu Nehemia tweve kwa kuwa karibu na walimu ambao wakumbwa na changamoto hiyo ,kwani amekuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanapata suluhu.

Bila kumung'unya maneno comrade Mwasanguti amampongeza RC wa Njombe kwa kusikiliza sauti ya ccm katika kutatua mgogoro huo pale alipopata taarifa.

Na kwa upande wao walimu wameonekana kuwekeza imani zaidi kwa ccm kwani wameona matunda kwa kipindi kifupi ambapo changamoto hiyo imewakuta na wameonekana kumpongeza RC wa Njombe comrade Olesendeka kwa maamuzi ya busara kukaa nao na kuzungumza kuhakikisha maslahi yao yanapatikana.

Je wajua,comrade mwasanguti ni mwepesi kubadilika kwa kusoma nyakati ili kuweza kumudu na kwa kuzingatia ubora wa kazi kulingana na jambo ,kwa maslahi ya jumuiya na jamii nzima.^

Hakuna maoni: