KATIBU WA MAKETE DEVELOPMENT ASSOCIATIN NA BALOZI WA NMB, AZUNGUMZA NA UMOJA WA WANAFUNZI WANAOSOMA DAR ES SALAAM VYUO NA VYUO VIKUU.
##Comred Award Mpandila
Ndg, wana makete wenzangu
Kwanza Niwashukuru kwa mwaliko huu
nimefurahi sana kuungana nanyi wanafunzi wa chuo kikuu mliotokea makete kwa
namna ya pekee mmepigana vita kwa miaka yote mliokua katka masomo yenu mmevuka
milima na mabonde.
Leo tupo hapa kama. Wana makete
tukifurahia umoja wetu huu kumbukeni kuna watu hapa wameacha majukumu yao na
wamekuja hapa kuungana na nyie sio kwamba hawana kazi la hasha ila wanawapenda
na Wanawajali kupita maelezo.
Umoja mlioishi shule usikome leo
hii, udumu katika damu zenu kuthamin makete kwanza kuliko kujitenga
ukitoka nje ya shule huku mtaani tunawakaribisha kuna chama
kinawaunganisha wanamakete kinaitwa MAKETE DEVELOPMENT ASSOCIATION (MDA),
mimi kama katibu mkuu, Naomba kama. Wapo hapa ambao hawajajiunga na MDA
wajiunge tuendeleze mapambano ya kuhakikisha makete inakua moja yenye umoja
bila ubaguzi wa aina yoyote, kwenye umoja wetu MDA tunakuwa wanachama
tunaoheshimiana bila kubaguana kwa nafasi zetu au vyeo vyetu tunaishi kama
familia moja, njia ya kujiunga ni raisi sana kwanza utatoa Kiingilio 10,000
/=tu hapo utakua mwanachama hai na wale wenye simu ambazo zina uwezo wa
Internet (whatsap) tutawaunga kwenye group ambapo mambo meng tunajadili
huko lakini umuhimu hata kwa wale wasio na simu tunawafikia taarifa mhimu
tunawatumia kwa njia ya kawaida ya Sandiku la barua, karibuni mjiunge kwenye
umoja wa wanamakete ( MDA)
Umoja huu uende mpaka kutafutiana
fursa za ajira kuna watu hapa wana uwezo wa kujiajiri wengine hawana uwezo huo
kuna wengne wana chanel za ajira tayar basi ukikuta kuna nafas sehem unamng'ata
sikio rafiki yako au kama wewe umeona sehem kuna kaz na unamjulisha mwenzako
huo ndo umoja unaohitajika
Na sisi kama. Watu tuliojiajiri
tunafahamiana na watu wengi kwenye makapuni na serikalini tutajitahid
kuwaunganisha na kazi hizo cha msingi mpeni cv zenu Kiongozi wenu ili kila
fursa inayopatikana tuwajulishe na tuisimamie muweze kuipata ajira
Lakin tunaomba mkawe wanyenyekevu
makazin wengi wetu hata mkitafutiwa kazi hamlindi heshima na kuiheshimu kazi
hivyo kwa wale watakaobahatika kupata kazi au kutafutiwa kazi lazima mkawe na
nidhamu kubwa kazini
Karibun mtaan shule mmejilinda na
UKIMWI na huku mtaan UKIMWI upo jiepushen nao msije mkapoteza nguvu kazi ya
taifa.
Mwisho niwashukuru wanafunzi wa vyuo
vikuu kupitia umoja huu mliweza kuchangia janga la moto mang'oto sec hakika
mliwafurahisha wana makete na MDA kwa ujumla wake
Nawakaribisha MDA pia nawatakia
mtihan mwema Mungu awabarik sana
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni