MBUNGE DEO NGALAWA AZINDUA ALBAM YA KWAYA KANISA TAG LUDENDE.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mkoa
wa Njombe Mh:Deo Ngalawa Mapema siku ya Tarehe05/07/2018 Amepokelewa na
wananchi wa Kata ya Ludende kijiji cha Ludende alipoalikwa kuwa Mgeni rasmi
katika Uzinduzi wa kwaya ya GLORY SINGERS YA KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF
GOD T.A.G.
Albam hiyo inakwenda kwa jiana NAPENDA Ambayo ni AUDIO Kwasasa wanatarajia
kufanya Shooting ya Video ifikapo Septemba mwaka huu na Uzinduzi huo umefanyika
katika Uwanja wa Kijiji cha Ludende.
Mheshimiwa Deo Ngalawa
ameichangia Kwaya hiyo fedha Taslimu kiasi cha Zaidi ya Shilingi Milioni moja
na nusu Tsh.1500,000/=
Pamoja na kuchangisha fedha nyingine
katika mkutano huo wa uzinduzi ambazo mheshimiwa Mbunge aliungwa mkono papo
hapo na baadhi ya wananchi walio hudhuria katika uzinduzi huo na kupata jumla
ya shilingi laki 5 Hivyo kwaya hiyo ya GRORY Ilijipatia Jumla ya shilingi
Milioni2 kwaajili ya Gharama ya Kushuti Video ya Albam yao ambayo imezinduliwa
rasmi yenye jina la NAPENDA,
Mheshimiwa Ngalawa pia akiwa
Ludende amefika katika Eneo linalojengwa KITUO CHA AFYA CHA KATA hiyo ambapo
ameona jitihada za wananchi wa Ludende zikiwa zinaendelea kwaajili ya Kujenga
jengo la MAMA NA MTOTO.
Katika kituo hicho cha afya ameahidi
kuendelea kuwaunga mkono ambapo tayari alishapeleka bati 45 za kuanzia na bati
ntingine zikiwa bado kuwapelekea kutoka kwenye ofis yake ili ziweze kukidhi
mahitaji katika majengo ya kuanzia.
Aidha Mheshimiwa Mbunge Deo Ngalawa
alipokuwa katika Kijiji cha Ludende alipata fursa ya kutembelea Taasisi
nyingine za kidini ambazo zipo katika shughuli za ujenzi wa Majengo ya kanisa
ambapo alitembelea katika Kanisa la ANGLICAN Ludende na kukuta waumini hao wapo
katika mchakato wa uwekaji wa Malumalu kwenye jengo la kanisa hilo.
Ngalawa ameahidi kuwaunga mkono ikiwa ni pamoja na
kufanya harambee ili kuweza kufanikisha kazi hiyo, Lakini Pia Mheshimiwa
Ngalawa alitembelea katika Kanisa La WAADVENTISA WASABATO Ludende na
kujionea waumini hao wakiwa wamejenga kanisa na kuliezeka bati likiwa
linasubiri hatua
za kulisakafia.
Mheshimiwa Ngalawa amewaahidi waumini hao wa
kanisa la WAADVENTISTA WASABATO Kuwaunga Mkono kwa kuwapatia smenti mifuko
hamsini 50, Mifuko hiyo ya sment amewahakikishia kuwa Mungu akiwajalia uzima
atawapatia Wiki chache zijazo ili waendelee kufanyia kazi.
Mheshimiwa Deo Ngalawa
amewaasa viongozi wa dini kuwakumbusha waumini wao kuhakikisha wanakuwa na
miradi ya vitega uchumi kwaajili ya kanisa ikiwa ni pamoja na kuanzisha mashamba
ya parachichi.
Samwel Shagama ni Mwenyekiti wa CCM kata
ya Ludende amewataka wananchi wote kuunga mkono jitihada zinazofanywa na
Serikali ya Chama cha mapinduzi CCM Bwana:Shagama Pia amemshukuru
sana Mbunge Deo Ngalawa kwa kukubali ombi la kuwa mgeni rasmi katika
taasisi za kidini na kuongeza kuwa yeye kama Mwenyekiti Wa CCM wa kata na
kijiji amefarijika sana kuona wananchi wake ambao wanajishughulisha
katika maendeleo ya Ujenzi wa makanisa kuwaunga mkono.
*HABARI NA
MATUKIO YA PICHA NA VASCO MGIMBA*
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni