Dstv Tanzania

CCM -NJOMBE WAMLILIA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM WILAYA YA WANGING'OMBE MAREHEMU JUMNNE KAPINGA.


R.I.P CDE KAPINGA.


Wingu zito na huzuni kubwa vimetanda ndani ya wilaya ya Wanging'ombe,mkoa wa Njombe ,wanachama wa CCM wote,Ndugu ,Rafiki na jamaa kwa msiba mzito uliotokea,kwa kumpoteza ndugu yetu jumanne kapinga kwa ajali ya pikipiki kwa kugongana na gari tarehe 06/07/2018 mida ya jioni,maeneo ya airport.

Baada ya ajali marehemu alikimbizwa hospitali ya kibena kuokoa uhai wake lakini ilishindikana kazi yake mola haina makosa.


   Marehemu Jumanne Kapinga Enzi za Uhai wake.

Marehemu ameacha mjane na watoto ,mwili wa marehemu umeagwa mtaa wa kwivaha tarehe 07/07/2018,Mkoan njombe na majira ya jion mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea songea
Marehemu alikuwa mzaliwa wa songea mazishi yamefanyika songea ,kata ya seedfarm ,mtaa wa unangwa ,leo tarehe 08/08/2018.

Viongozi mbalimbali wa dini, vyama vya siasa na serikali wameungana na ndugu ,jamaa na marafiki kumsindikiza marehemu katika nyumba yake ya milele

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akizungumza na Waombolezaji.
   "Hakuna aijuaye kesho na kazi yake mola haina makosa"Ndivyo unaweza Kusema  kwani Tuliamini tutakuwa naye kila siku lakini Mungu anamipango yake.


Marehemu kapinga amewahi kuhudumu kama katibu msaidizi wa wilaya ya Njombe ,na Baadaye aliteuliwa kuwa katibu wa ccm wilaya ya Wanging'ombe mpaka pale umauti ulipomfika.
Maelfu ya Wananchi wa Songea Waliojitokeza Kumsindikiza Ndugu yao.
Katika utumishi wake ndani ya wilaya hiyo marehemu alisimamia uchaguzi na viongozi wenzake 2015 na walipata ushindi wa nguvu bila kupoteza jimbo wala kata vyote ni ccm hakika alitufaa sana wana CCM.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Ndg Hosea Mpagike akitoa Salamu za Pole,Kulia kwake ni katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Njombe Bwana Erasto Ngole
Lakini pia maisha yake hayakuishia CCM tuu alishiriki vyema shughuli za kijamii ,shabiki mkubwa wa mpira wa miguu na alikuwa shabiki wa timu ya simba .
 
  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wanging'ombe.
 Katika Salamu zake za Pole Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Wanging'ombe Kinyangadzi amesema Chama cha Mapinduzi Wilayani humo kimepata pigo kubwa kwa kumpoteza Mtu aliyekuwa Muhimu katika ujenzi wa Chama kwani alikuwa mtu mwenye kujituma na Kuwajibika ipasavyo kila alipohitajika katika jamii.
Mwili wa Marehemu ukishushwa Kaburini
Sifa kubwa za utendaji wake ulidhihirisha dhahiri kwa muungano uliopo ndani ya wilaya ya wanging'ombe pindi linapotokea jambo liwe la furaha na huzuni wanawanging'ombe wamekuwa wamoja sana hakika kapinga ulitufaa sana lakini Alipangalo Mungu binadamu huwezi kulipangua.

 Mmoja kati ya Makada Maarufu  wa CCM Mjini Njombe akiwa katika Eneo la Msiba.
Pole ccm.....
Pole wanging'ombe....
Pole ndugu ,rafiki,jamaa na mashabiki wa mpira.


Ndugu yetu hatunaye tena ,Tumuombee kwa Mungu apumzike kwa amani.

Imeandikwa na Titho Stambuli. 

Tazama Picha Zaidi Hapa Chini>>>



Mwili wake Ukishushwa Kaburini

Hakuna maoni: