MWKT WA UWT WILAYA YA NJOMBE,AIBUKIA KWENYE MAPOKEZI YA NDEGE AINA YA BOEING 787-8 DREAMLINER ,UWANJA WA NDENGE.
Na stambuli titho
Leo Tar 8/07/2018
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya
Njombe Bi Angela Mwageni,amepongeza na kusifu zoezi la kupokea ndege mpya
iiyowasili July 8/2018 katika uwanja wa
ndege DSM (Mwalimu Nyerere International Airport).
Mwkt huyo mwenye maskani yake
Wilayani Njombe , anayesifika kwa kujitolea na kuwajibika katika majukumu ya
kijamii wilayan Njombe mahala popote ambapo amekuwa akipewa nafasi ameonekana
kumudu nafasi zote na hivyo kuwa nguzo kubwa katika jamii.
Amewaomba watanzania kumuombea raisi
wetu ili azidi kuhakikisha taifa letu linapata maendeleo kwa maslahi ya
watanzania na kuliombea taifa letu Aman,Yeye kama kiongozi na raia wa
Tanzania anavutiwa na kasi ya mheshimiwa raisi kwa kuliletea maendeleo
taifa .
Mwangeni amewataka watanzania
kutambua usafiri wa anga ni mhimu katika taifa letu ilikuweza kutanua wigo wa
biashara za kimataifa ,utalii na kukidhi matakwa mengine kufuata huduma za
kijamii nje ya nchi ,kupitia yote hayo itasaidia pia kukuza uchumi wa taifa
letu.
"ili biashara na viwanda vikue
ni lazima miundombinu iwe imara ili watanzania waweze kusafirisha malighafi zao
nje ya nchi na kukuza utalii"
Amepongeza pia ujenzi wa reli ya
kisasa ambapo italeta ufanisi mkubwa katika sekta ya viwanda na usafiri kwa
kuwa ni usafiri ambao utakuwa unatunza muda na kusafirisha malighafi na bidhaa
sehemu mbalimbali nchini.
Hivyo yeye binafsi anaguswa na
mafanikio hayo na ndio maana ameona afike Airport kuungana na mheshimiwa raisi
kupokea ndege hiyo kwa kuwa anatambua umuhimu wake kwa taifa letu.
Aidha amepongeza chama cha mapinduzi
kwa kuwa kimekuwa nguzo ya kupata viongozi wenye moyo wa kweli katika
kuhakikisha taifa linasonga mbele,amewaomba watanzania kuendelea kuunga mkono
wa juhudi za raisi magufuli na CCM kwa kuwa maendeleo yanayofanywa yanaonekana
na pia CCM na raisi Magufuli wameonekana kukemea rushwa na ufisadi ili kuweza
kuondoa matabaka nchini na kila mmoja kunufaika na keki ya taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni