AFISA MTENDAJI WA KATA YA LUDENDE AONGOZA TEAM YA KAMATI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KWENYE MIKUTANO YA HADHARA YA KILA KIJIJI KWENYE KATA YAKE.
Ili kuhakikisha Uharakishaji wa
Ujenzi wa Kituo cha afya katika kata ya Ludende Wilayani Ludewa Afisa
Mtendaji wa Kata ya Ludende Bwana Heyrimus Mtega amekuwa anafanya ziara
ya kuiongoza Kamati ya UJENZI WA KITUO CHA AFYA YA KATA Pamoja na
Wenyeviti na watendaji wa Vijiji vyote vilivyopo katika Kata ya Ludende.
Vijiji vinavyounda kata hiyo ni pamoja na Maholong'wa,Madindo na,Ludende huku Lengo la ziara hiyo ni
kuitambulisha Kamati iliyoundwa na Serikali zote 3 kwenye KAMAKA
iliyoketi siku chache zilizopita.
Lakini pia Ziara yake ilelenga kupeana mikakati iliyoafikiwa
na Kamati hiyo ikiwemo kutoa Michango ya fedha kila mwananchi wa kata ya
Ludende ili ziweze kusaidia shughuli ya Ujenzi wa Jengo la Mama na
Mtoto.
Siku ya Tare 12/07/2018 Kamati hiyo ilishiriki Mkutano wa
Hadhara katika Kijiji cha Ludende na kutoa maazimio hayo kwa Wananchi na
wananchi wa Ludende wameipokea vizuri swala la kuendelea kuchangia
michango hiyo papo hapo katika Mkutano huo wananchi pamoja na viongozi
walianza kutoa michango yao na kupatikana kiasi kisichopungua laki4,.
Katika Mkutano huo pia ambapo Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Samwel
Shagama aliyeongoza zoezi la kukusanya fedha hizo alipokea mchango
mwingine wa fedha kutoka kwa Wanafunzi wanaofanya mafunzo ya vitendo
katika Katika Zahanati hiyo ya Ludende ambayo sasa imepandishwa hadhi
kuwa kituo cha afya,toka chuo cha Uuguzi cha HOSPITAL YA LUGARAWA nao
waliunga mkono wananchi hao kwa kutoa fedha kidogo.
Lakini pia katika Mkutano huo ulikuwa na agenda nyingine za kusoma
mapato na matumuzi.
Pia walialikwa wataalam mbalimbali waliopo katika
kata hiyo Akiwemo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya
Ikovo Bwana Faustin Mgimba pamoja na Mratibu elimu wa Kata hiyo Bwana
Athanasi Kibena nao wakatumia nafasi hiyo Kuwakumbusha wazazi na walezi
kuhakikisha wanatoa ushirikiano mzuri kwa walimu wao ili kuwa jirani na
maendeleo ya wanafunzi wao, pamoja na kuwashukuru kwa kambi lililokwisha
kupita mwezi Jun,-Agost.
Mkutano huo
unaendelea tena katika Kijiji cha Madindo ambapo siku ya
tarehe13/07/2018 Afisa mtendaji wa kata ataiongoza kamati yake ya Ujenzi
Kwani mwanzo wa Mkutano huo ulikuwa ni kijiji cha Maholong'wa siku ya
Tarehe11/07/2018.
Lengo ni kuhakikisha ujenzi wa jengo la Mama na mtoto unakwenda kwa kipindi miezi 3 na sivinginevyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni