KATIBU MWENEZI CCM MKOA WA NJOMBE ASEMA KOMBE LA DUNIA NI FUNZO KWA AFRIKA,ANASEMA WAAFRIKA TUNAHITAJI KUWA NA MPANGO WA MUDA MREFU ILI KUFANIKIWA KATIKA SOKA.
Na stambuli titho
Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa
Njombe comrade Erasto Ngole ,umahiri wake katika siasa pia katika michezo yeye
ni mpenzi sana wa mpira wa miguu na yeye nchini Tanzania ni shabiki haswa wa
klabu ya yanga.
Katika kipindi hiki amekuwa
mfuatiliaji mzuri wa kombe la dunia kwani ndio burudani yake kubwa ,lakini
ameonekana kusikitishwa namna timu za Africa zilivyosukumizwa nje mapema katika
michuano hyo yeye kama mwafrica mwenzao imemgusa sana na kwa kuwa imekuwa kama
desturi kwa waafrica kushindwa kujinasua katika hilo.
Ameshauri vyama vya mpira kuanzia
ngazi ya wilaya ,mkoa,taifa ,ukanda na mpaka bara zima kuhakikisha wanapanga
makakati wa kukuza soka na hatimaye kuondoa aibu hii ambayo imezidi kutukumba
pindi mashindano hayo yanapofanyika,yeye kama mdau wa mpira anashauri kuwe na
mpango wa mda mrefu kuhakikisha wanafikia mafanikio hayo ya kisoka.
"vyama vya mpira vinatakiwa
kuwa na misingi ya elimu ya michezo kuanzia shule za msingi,kuandaa academy za
michezo,kuwatumia wadau wenye nia na waliofanikiwa katika soka ili kuweza
kufikia malengo mazuri na kuandaa watalaami watakao kuwa na uhakika katika
kukuza soka."
Lakini kiongozi huyo bado anaamn
viongozi watajipanga na kuhakikisha Africa wanafika mbali kisoka .pia
amepongeza timu za Africa magharibi mara kadhaa wamejaribu kuonyesha jambo
katika mashindano ya kombe la dunia licha ya kuwa wamekuwa hawafikii malengo.
Aidha pia amegusia kwa soka la
Tanzania ameomba ni maandalizi ya uhakika yazidi kufanyika kila wakati na kuwa
na mpango wa mda mrefu .
Bwana Ngole Amegeukia pia mkoa wa Njombe hususan
Njombe mji na kudai kuwa wananjombe hawajakata tamaa na timu yao na wataendelea
kushirikiana nao kuhakikisha tunairudisha ligi kuu na kurudi katika ramani ya
mpira ,kwani wananjombe walipata mahala pakukutana pamoja na kuburudika na
kuzidi kuwa na mshikamano katika soka hivyo ni vyema timu yetu ya Njombe
ikarudi na tukaendelea kuona mafanikio yake kwa kuwapa ajira vijana ,michezo ni
afya na burudani pia.
Kuelekea Kumalizika kwa Michuoano ya Kombe la Dunia Croatia wameingia fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika
historia, baada ya kuichapa England 2-1 katika mchezo ambao ulichezwa
kwa dakika 120.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni