Dstv Tanzania

MAKAMU MWENYEKITI CCM BARA, NDG.PHILIP JAPHET MANGULA ATEMBELEA MAONESHO YA 42 YA KIMATAIFA SABASABA.



Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Philip Japhet Mangula Leo tarehe 12/07/2018 ametembelea Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa Katika Viwanja Vya Sabasaba yaliyopo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere wilayani Temeke ili kujionea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Mkuu 2015/2020 ulivyo kwenye maonesho hayo.

Makamu Mwenyekiti alipokelewa na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Ndg.Edwin Rutageruka ambaye alizungushwa kwenye mabanda mbalimbali ya viwanjani hapo yakiwemo banda la NSSF, banda la Chuo kikuu Cha Kumbu Kumbu ya Mwalimu Nyerere, banda la JKT,  banda la TBC, banda la mamlaka ya Chakula Tanzania, 


Akiwa katka banda La NSSF Makamu mwenyekiti Bara amempongeza Mkurugenzi wa NSSF, Prof Kyalala kwa Kazi kubwa na nzuri anayoifanya Lakini pia amemsisitiza Mkurugenzi kujenga Viwanda na kuimarisha Mifuko ya Wakulima na wafugaji ili kuwakomboa Watanzania kiuchumi ikiwa ni Sehemu ya maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu 2015/2020.

Baada ya ziara hiyo Makamu Mwenyekiti Bara Katika majumuisho mara baada ya kutembelea maonesho hayo Ndugu Mangula amesifu Uongozi Mzima wa TANTRADE kwa maonesho ya mwaka huu yamejaza Wafanyabiashara Wazalendo wengi, pia amefurahishwa na fursa mbalimbali za kiuchumi na ajira Lakini ameshauri maonesho hayo yafanyike kwa kuwasaidia Watanzania Hasa wale wa hali ya Chini ili kuwainua kiuchumi. 

“Utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi mjikite kuimarisha na kuboresha Viwanda Vyama SIDO ili kuongeza Ajira kwa Vijana na Watanzania kwa Ujumla. Maonesho kama haya tuzidi kuyaboresha kwa ufanisi Mkubwa mnoo hasa kutanua wigo wa ajira na biashara.


Pia Makamu Mwenyekiti amefurahishwa snap na utaratibu  wa kuwa na matukio mbalimbali kila siku kwenye maonesho hayo. 

Matukio hayo ni kuwa na siku ya mazingira,  rushwa, asali, sanaa na utamaduni ambayo yalishirikisha jumla ya Watu 2560.

“Malengo ya ilani ya uchaguzi wa 2015/2020 yamejikita zaidi kuwakomboa Watanzania kiuchumi na Kimaendeleo.


Katika msafara wake aliongozana na Maafisa mbali mbali kutoka Ofisi Ndogo  ya CCM Makao Makuu Lumumba.

Imetolewa na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Lumumba 
12Julai,2018

Hakuna maoni: