HALMASHAURI KUU CCM WILAYA YA NJOMBE YAKUTANA KUJADILI UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA 2015-2020 KWA KIPINDI CHA JULAI HADI DESEMBA,2017.
Na stambuli titho,13/07/2018.
Halmashauri kuu CCM wilaya ya Njombe imekutana leo kuhakikisha inapewa taarifa ya wilaya ya Njombe kuhusu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm 2015-2020 kwa kipindi cha julai hadi Desemba,2017.
Halmashauri kuu hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa wilaya hiyo mwkt wa ccm wilaya ya Njombe Edward Mgaya na mtendaji wake wa chama Antony katani, huku upande wa viongozi wa serikali ukiongozwa na DC comrade Ruth Msafiri na pamoja na wenyeviti wa halmashauri na wakurugenzi wa halmashauri.
Huku viongozi wa ccm mkoa wa Njombe wakihudhuria halmashauri hiyo -Katibu wa ccm mkoa wa Njombe Ndugu Hosea mpagike ambaye ameongozana na katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe comrade Erasto G Ngole(Shikamooparachichi),Mwkt wa UWT mkoa wa Njombe Bi Mary Lwiva na mwkt wa uvccm mkoa wa Njombe ndugu Nehemia Tweve.
Ambapo serikali imeweza kuwasilisha Taarifa yake ya kiutendaji ambayo inatekelezwa kwa mujibu wa ilani ya ccm ambayo waliinadi kwa wananchi wakati wa kuomba kura,kila halmashauri zote tatu zimeweza kuwasilisha taarifa kupitia wakurugenzi na wakuu wa idara.
Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akifuatilia Kwa Makini Kikao hicho. |
Taarifa hiyo ambayo imeonyesha mafanikio na changamoto mbalimbali zilizochangia kutokufanikiwa kwa baadhi ya miradi katika kila halmashauri makambako ,Mji Njombe na wilaya ya Njombe ,idadi ya watu wilaya ya Njombe 309,797 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi 2012.
Ambapo taarifa hyo imeweza kugusa kada zote Elimu,Afya,maendeleo ya jamii,Ardhi na miundo mbinu mfano barabara.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe. |
Katika elimu wataalamu wameweza kutoa taarifa ya ongezeko la ufaulu ,kwani jitihada kila siku zimezidi kufanyika ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika pande zote mbili msingi na sekondari,idadi ya shule za msingi serikali 163,private 13 jumla 176 , na sekondari 56 ,serikali 34 na private22. changamoto upungufu wa walimu,utoro ,ongezeko kubwa la wanafunzi,mahusiano mabovu baadhi ya shule na jamii,uvamizi wa maeneo ya shule za msingi na uwepo wa walimu wasionauwezo kufundisha..katika kuhakikisha utatuzi wa changamoto hizi wataalamu ,wadau na ofisi ya mkurugenzi kuhakikisha wanatafutia majibu changamoto hizo.
Mwenyekiti wa UWT-CCM Mkoa wa Njombe Bi Rosemary Lwiva akifuatilia Kikao Hicho. |
Ambapo taarifa imeeleza uimarishwaji na kusogeza huduma karibu kwa wananchi ,kwani jitihada kubwa imewekwa na serikali na wananchi katika kuboresha huduma za Afya hadi vijijini na huduma ya dawa na watalaamu wanapatikana kwa 95%.
Chanamoto-upungufu wa madaktari ,mwitikio mdogo wa kujiunga na Bima na Afya CHF/TIKA na mtazamo hasi wa tohara kwa vijana na watoto wote.
Utatuzi wa changamoto hizo ni wananchi wanahamasishwa kushirikishwa ujenzi wa Afya ,kuajiri madaktari na utoaji wa elimu.
Meza Kuu; Wa kwanza ni mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Edward Mwalongo,Katibu wa CCM wilaya ya Njombe,Mwenyekiti CCM wilaya ya Njombe,mkuu wa wilaya ya Njombe na katibu mwenezi Erasto Ngole. |
Huduma bora za maji ni nyenzo msingi katika kuondoa umaskini na kuharakisha maendeleo ,hadi sasa upatikanaji wa maji kwa vijijini na mijini bado ni ya wastani na wakati wa kiangazi hairidhishi hasa mijini .
Changmoto-miradi ya mjini changamoto haina uwazi ,uharibifu wa mazingira ,vyanzo vya maji na miundombinu
Utatuzi -wataalamu wameahidi ufuatiliaji wa karibu na kuchukua hatua,upandaji miti,kuelimisha wananchi na kupambana na uharibifu wa mazingira.
Moja ya Kablasha lililosheheni Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi |
Kata 36 kati ya 37 zinajishughulisha na kilimo cha biashara na chakula ,kilimo kimeeliekezwa kusimamiwa na ushirika hasa mazao ya kimkakati chai na kahawa,kazi inayoendelea kukamilishwa ,aidha wilaya yetu ina mazao ya biashara na chakula ambayo ni miti,viaz ,mahindi ,matunda(parachichi).Mazao haya yameonekana kuwaingizia kipato wananchi na kupata chakula.
Chanagmoto-zinazoathiri kilimo ni ucheleweshwaji wa pembejeo ,Baadhi ya watu kuzoroteha ushirika ,changamoto ya soko na vipimo kupunja wakulima(. lumbesa ).
Utatuzi-upatikanaji mapema wa pembejeo,kuimarisha ushirika na wakulima kujiunga,kulima kwa kuzingatia ushauri wa maafisa kilimo.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali Kutoka Halmashauri ya Mji Njombe. |
Ufugaji wa Ng'ombe wa maziwa ni mojawapo ya eneo lenye kuleta kipato kwa wafugaji na mafanikio ni kuwepo kwa kiwanda cha maziwa NJOLIFA ikiwa ni utatuzi wa soko la maziwa
Changamoto-idadi ya wafugaji bado ni ndogo ,bei ya maziwa hairidhishi na ufugaji wa mazoea na uchache wa maafisa ugani.
Utatuzi -kuendelea kutoa elimu kwa wafugaji,kuongeza wataalamu na kuhamasisha wafugaji hasa vijana.
Aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruthi Msafiri |
Serikali inaendelea kutekeleza sera ya taifa ya uwezeshaji kiuchumi kwa kuanzisha mpango wa kukabiliana na umaskini hasa kwa vijana (wanawake na watu wenye ulemavu).
Mafanikio-utoaji wa mikopo kwa fedha hizi ni mzuri.
Changamoto-fedha ni kidogo kulingana na mahitaji,urejeshaji hafifu hasa vijana na Baadhi ya wanakikundi kukosa uaminifu.
Ardhi ,mazingira na miundombinu kama vile barabara serikali imetoa taarifa kuwa usimamizi ni mzuri kwa kishirikiana na wadau ,wataalamu na pamoja na serikali kuhakikisha hivi vyote vinakuwa sawa kwa maslahi ya wanachi ili kuweza kupata maendeleo.
Aidha ccm imepongeza mafanikio hayo na kuhakikisha changamoto zinazofifisha maendeleo kwa jamii ziweze kutatuliwa ili kuhakikisha maendeleo yanawanufaisha wananchi wa wilaya ya Njombe.
Tazama Picha zaidi Hapa Chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni