Na
Erasto Mgeni,Njombe.
|
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Akitolewa Damu Tayari kwa Kupima Afya Yake. |
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe Ndg.Comred Erasto Ngole Ni miongoni mwa Viongozi wa CCM Mkoa wa Njombe walioshiriki Kikamilifu
Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya “FURAHA YANGU”Inayolenga kuhamasisha jamii
kupima Virusi vya UKIMWI Kwa hiari na Kuanza Kutumia Dawa za Kufubaza Makali
ARV’S.
Kampeni hiyo Kwa mara ya
Kwanza Ilizinduliwa rasmi Juni 19 mwaka
huu mkoani Dodoma na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim
Majaliwa na inaratibiwa na Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Tume
ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS).
Mkoa wa Njombe Umekuwa
Mkoa wa Pili Kuzindua Kampeni hiyo katika Sherehe zilizofanyika Viwanja vya
Mt.Bakita Njombe Mjini Huku Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christophwer Ole Sendeka
Akiwa ndio Mgeni wa Heshima katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Hali Kadhalika Uwepo wa
Viongozi wa Juu wa Chama cha Mapinduzi katika Mkoa Wa Njombe katika Uzinduzi huo Umeonyesha Dhahiri Kuwa
Chama hicho kipo pamoja na Serikali yake
katika Kuhakikisha kuwa Jamii yake Inakuwa na Afya Njema Hususani katika
Mapambano ya Maambukizi Mapya ya Virusi vya UKIMWI.
|
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Aliposimama kutambulishwa. |
Mh.Erasto Ngole Maarufu kwa jina la Shikamoo Parachichi
akitamba na Kauli Mbiu yake ya ‘MTONYO UTAUPATA SHAMABANI’ alijizoelea Umaarufu hivi Karibuni kwa uwezo wake wa Kuhamasisha
wananachi wa Mkoa wa Njombe Kujikwamua kiuchumi kwa Kulima Parachichi huku yeye
mwenyewe akionyesha Mfano ameonekana Kuwa na Furaha alipohudhuria Uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mara baada ya Mkuu wa
Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka Kuzindua Kampeni hiyo Bwana Erasto Ngole
Alikuwa mtu wa Kwanza Kupima Mambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Moja ya
Banda lililokuwepo Eneo Hilo.
|
Comred Erasto Ngole akijiandaa Kupima Afya Yake. |
Kamera za Waandishi
zimemshuhudia Bwana Ngole akiwa Mstaari wa Mbele kuwahamasisha Vijana,Wanawake
na wanaume Kushiriki kikamilifu katika zoezi la Kupima Afya zao.
Viongozi wengine
walioshiriki Uzinduzi wa Kampeni hiyo ni Pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe
Hosea Mpagike, Katibu Hamasa na Chipukizi mkoa wa Njombe Johnson Elly
Mgimba,Katibu wa Hamasa Wilaya ya Njombe Iman Moyo,Sadock Mwanda Huyu ni Kada
Maarufu Kutoka Songwe, Daniel Muhadza Katibu wa UVCCM Wilaya ya Njombe, na
Ndugu Chone kutoka UVVCCM Mkoa wa Njombe Kama Baadhi yao wanavyoonekana katika
Picha Hapa Chini.
|
Erasto Ngole Katikati Akiwa Amesimama na Baadhi ya Viongozi wa CCM,Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Akiwepo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mwenye Suti ya Bluu. | | |
|
Johnson Elly Mgimba Katibu Hamasa na Chipukizi mkoa wa Njombe | |
|
Imani Moyo Katibu Hamasa na Chipukizi wilaya ya Njombe |
|
Sadock Mwanda Huyu ni Kada
Maarufu Kutoka Songwe |
Awali Akizindua Kampeni hiyo mkuu
wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amewaagiza wakuu wa wilaya za Mkoa wa Njombe kuhakikisha wanasimamia na kuendesha kampeni
ya kupima Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa hiari kwa watu wote hasa wanaume katika
mikoa yao na wilaya zao.
|
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia Uzinduzi wa Kampeni ya 'FURAHA YANGU' Katika Viwanja vya Mt.Bakita. |
Olesendeka Amesema, viongozi hao
wanatakiwa kutumia miezi hiyo kuhakikisha wanasimamia na kusambaza kampeni hiyo
mfululizo hadi vijijini pamoja na kutoa taarifa mwenendo wa kampeni hiyo kila
mara katika ofisi yake.
Amewataka wahakikishe wananchi
wote hususan wanaume wanapima afya zao na kutumia Dawa za Kufubaza makali ya
virusi (ARVs) sawia.
Takwimu Zinaonyesha Kuwa hadi sasa Watanzania asilimia tano tu ndio
wameambukizwa na lengo ni kuhakikisha asilimia 95 waliobaki wanapima kujua afya
zao.
|
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka mapema leo Akikagua Banda la watoa Huduma za Afya,Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri |
Ole Sendeka amesema mkakati wa
serikali ni kuhakikisha wanaume wako mstari wa mbele kupima na kujua afya zao
kwa sababu takwimu zinaonesha kwamba wamekuwa mstari wa nyuma kupima.
|
Viongozi wa Serikali,Wadau wa Afya Pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika Picha ya Pamoja Mapema Leo. |
Upimaji huo unalenga kwenda na
Dira ya Taifa ya kuwa na Tanzania bila Ukimwi kutokana na kuridhia malengo ya
UNAIDS ya 90-90-90.
Malengo ni asilimia 90 ya watu
wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao, asilimia 90 ya wenye maambukizi kuanza
dawa na asilimia 90 ya walioanza dawa kufaulu kufubaza mwili.
Zaidi Tazama Matukio Katika Picha Hapa Chini
|
Wakuu wa Wilaya za Makete,Ludewa,Wanging'ombe wakipewa maelekezo na Mtaalamu kabla ya Kupimwa afya zao,Pembeni ni Katibu Mwenezi wa Cccm mkoa wa Njombe Erasto Ngole |
|
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Comred Ally Kasinge Akiwa tayari kupimwa Afya yake. |
|
Sehemu ya Umati wa Wananachi wakiwemo wanafunzi wa Sekondari waliofika Kushuhudia Uzinduzi wa Kampeni ya Furaha yangu |
|
Christopher Ole Sendeka Mkuu wa Mkoa wa Njombe Akinyanya Mkasi tayari kwa kukata Utepe. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni