ZIARA YA MH.MPOGORO NA KATIBU WA WAZAZI MKOA WA NJOMBE YASIMAMISHA SHUGHULI WILAYANI LUDEWA.
Mwenyekiti jumuiya ya wazazi CCM mkoani Njombe Cde-Josephat
Mpogoro Akipokelewa na Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Ludewa Ndugu John Kiowi |
Na Titho Stambuli,Njombe.
Nguli wa siasa mkoani Njombe,ambaye
amebeba dhamana ya kuongoza jumuiya ya wazazi mkoani Njombe Cde-Josephat
Mpogoro akisaidiwa na mtendaji wa jumuiya hiyo Cde-Lucas Nyanda ,wameanza ziara
hyo leo 17/07/2018, Katika kata ya madobe na madilu.
Baada ya kulakiwa na
mwenyeji wake ambaye ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Ludewa Ndugu John Kiowi na katibu wake Bi Veronica Biria,viongozi hao waliweza kupata
taarifa ya kiutendaji na hali ya kisiasa wilayani Ludewa kutoka kwa viongoz
ngazi wilaya na kuzungumza na viongozi wa jumuiya hyo ngazi ya kata wakiwa na
Diwan wa kata hyo Polycarp Mlelwa na Diwan vitimaalumu Avelina Mgaya.
Ambapo katika taarifa iliyotolewa na
katibu mtendaji wa wilaya hyo Bi abiria ameeleza kuwa hali ya kisiasa wilayan
humo ni shwari na kunaushirikiano mkubwa kati ya wanachama na jumuiya ,na
kuhakikisha jumuiya inakuwa na nguvu,na Pia yeye kama mtendaji anashilikiana
vizuri na viongozi ,pamoja na mwkt wake kuhakikisha jumuiya inasonga mbele kwa
maslahi ya ccm na taifa letu.
Ameweza kumweleza mwkt wa wazazi miradi ambayo
inasimamiwa na jumuiya hiyo inakwenda sawia licha ya changamoto zilizopo ,mirad
inayosimamiwa wilayan ludewa ni pamoja na shule za sekondari Ludewa sekondary
na Masimbwe ,wao kama wazazi kwa kutambua kazi mchango wao katika jamii hasa
kipengere cha elimu na malezi hivyo wanamajukumu ya kuhakikisha wanasimamia
shule vilivyo ili swala la malezi kwa watoto liendelee kuwa imara na hivyo
kuwataka wazazi waendelee kuungaa mkono juhudi za jumuiya hyo wilayan Ludewa.
Baada ya kupokea report hyo ,Mwkt wa
wazazi mkoa wa Njombe ndugu Josephat Mpogoro amewapongeza viongozi wa wilaya
hyo kwa kuonyesha utendaji kazi unaoendana na kasi ya raisi wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania,lkn pia ameweza kuwaomba wazazi kuweza kushikamana na
kuhakikisha ccm inazd kuwa imara.
Mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Njombe ndugu Josephat Mpogoro akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya ya Ludewa. |
Amegusia swala la malezi kwa wazazi ni jambo
kuzingatia ili kuhakikisha jamii inakuwa na maadili ili kuwa na kizazi chenye
heshima na chenye mafanikio,amegusia pia swala zima la elimu kwamba ni lazima
wananchi wa lidewa waamke na wasidhani ni jambo la mchezo Elimu ndio mkombozi
pekee katika jamii zetu akitolea mfano miradi mikubwa inayotarajiwa kunzishwa
wilaya ya ludewa ni lazima ije isimamiwe na watoto wetu hivyo ni lazima wafike
mpaka chuo kikuu waje kuhakikisha wanalinda rasilimali hizi.
Kiongozi huyo ameonekana pia
kukazia zaidi swala zima la uchumi katika ziara yake ,kwani anaamn bila uchumi
hakuna jambo litakalo kwenda ,ni lazima wazazi wajitathimini kuhakikisha
jumuiya inakuwa na miradi ametoa mfano wa kilimo ndani ya kata ya madobole na
madilu kwamba walime chai,parachichi na mikorosho ili waweze kuwa na uchumi
mzuri kuanzia ngazi ya familia mpaka chama na kufanya kuwa muunganiko wenye
nguvu.
Aidha amewaomba wazaz kuhakikisha
wanashirikiana na jumuiya zote ili kuweza kuhakikisha ccm inashinda kata zote
na kurudisha kata ya madilu ,pia ameahidi kwa kushirikiana na wanaccm ,wadau
mbalimbali kupitia ofisi yake watajipanga kuhakikisha wanatatua changamoto
zinazoathiri miradi ya jumuiya ya wazazi kama vile shule nk ili kuongeza
ufanisi na kutoa huduma nzuri kwa jamii.
Katibu wa jumuiya hyo hakuwa mbali
na maelezo ya mwkt wake ,kwanza kabisa amemshukuru mwkt wake kwa kuamua kufanya
ziara ya kuimarisha jumuiya hyo kwa kushuka kuonana na viongozi ngazi ya chini
ni hekima na busara kwa kiongozi mkubwa kama huyo kufika huko.
Naye kwa
upande wake ameonekana kukerwa na mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii kwani
bila maadili hakuna maendeleo wala mambo ya msingi,Hivyo wao kama wazazi hawana
budi kuhakikisha swala la malezi linakuwa sawa ili kuepukana na mimba za
utotoni,utoro shuleni jambo ambalo linadhoofisha kiwango cha elimu,na uvivu wa
ufanyaji wa kazi.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Njombe Cde-Lucas NyandaAkizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya ya Ludewa. |
Katibu huyo mwenye hekima na busara
mjini Njombe amewataka wanachama wa jumuiya ya wazazi kujitathiminj hali ya
uchumi waliyonayo kwani hairidhishi ndani ya jumuiya na hivyo kupunguza nguvu
ya utendaji na pia mwenendo wa hali ya uchumi kuanzia ngazi ya familia
hairidhishi hivyo wajikite kusimamia hilo ili wawe na nguvu ya kuhudumia na
kusimamia jamii nzima kwa ujumla.
Aidha wananchi wa kata hizo
wamepongeza ujio wa mgeni huyo kwakuwa wameweza kupewa maarifa mbalimbali ya
kuimarisha jumuiya ya wazazi ,maisha ,na hasa swala zima la uchumi .pia madiwan
wa kata ya Madope Polycarp Mlelwa na Avelina Mgaya -Diwan vitimaalumu ambao
kimsingi wanahudumu mpaka kata ya madilu kwa vile iko upinzan wameweza
kupongeza ujio wa viongoz hao na watayafanyia kazi maagizo yao na wataendelea
kutoa ushirikiano wa hali ya juu.
Zaidi Tazama Matukio Katika Picha hapa Chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni