MWENYEKITI WA WAZAZI-CCM NA KATIBU WAKE MKOA WA NJOMBE WATEMBELEA SHULE YA WAZAZI SEKONDARY MASIMBWE -LUDEWA.
Na titho stambuli.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi-CCM
Mkoa wa Njombe Mh.Mpogoro leo tarehe 18/07/2018,amefanya ziara katika shule ya
sekondari ya masimbwe inayomilikiwa na jumuiya ya wazazi -ccm,ambapo ameweza
kukagua miradi mbalimbali iliyopo shuleni hapo na kupata taarifa ya jumla ya
shule ya kiutendaji.
Shule hiyo yenye kufundisha masomo
ya ufundi (umeme,magari,kushona nguo) ,ufugaji(kuku,ng'ombe),na elimu ya
sekondari,vyote hivi vinafundishwa shuleni hapo ,mwanafunzi anaweza pata elimu
mbili kwa wakati mmoja elimu ya kawaida ya sekondari na ufundi pamoja na
ufugaji au kuchagua,
Hii ni moja ya shule nzuri nyanda za juu kusini zenye
kuweza kumuandaa kijana aendane na kasi ya viwanda na pia kumfanya asiwe na
changamoto ya ajira anaweza kujiajiri mwenyewe,pia sifa nyingine ya shule hiyo
ni pamoja kuwa na kila aina ya vifaa vya kumfundishia mwanafunzi vifaa vya
maabara na ufundi hivyo kumamfanya mwanafunzi aweze kujifunza vizuri.
Bodi ya shule ya masimbwe imeweza
kumuonyesha miradi ya shule,vifaa vya kufundishia ,mifugo ambayo inafugwa
shuleni hapo(ng'ombe,kuku,nguruwe na ufugaji wa samaki).
Baada ya kutembelea miradi hiyo mwkt
wa wazazi mkoa wa Njombe amekutana na wajumbe wa Bodi ya shule na kuzungumza
nao juu ya maendeleo ya shule hiyo.
Ambapo kikao hicho kilifunguliwa na
mwkt wa bodi hyo ya shule na kufuatiwa na mkuu wa shule kutoa taarifa ya
mwenendo wa shule hyo.
Ambapo katika taarifa hyo amemweleza
mwkt kuwa hali ya shule ni nzuri walimu wapo,ufaulu umeongezeka kwani mwaka huu
kiwilaya imeshika nafasi ya 6 katika shule 23,pia wadau mbalimbali kutoka ndani
ya Tanzania na Nje ya Tanzani,licha ya kuwa na ufaulu mzuri na vifaa ya
kutosha vya kufundishia ,changamoto ndogondago hazikosekan na wanashilikiana na
wajumbe wa bodi kuhakikisha wanaendelea kuzitatua .
Baada ya kupokea ripot hyo Mwkt
akapata nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa bodi hyo kuona ni namna gani
wanaweza kuiimarisha zaidi na miradi hiyo kuzalisha kwa wingi kwa maslahi ya
shule maana inasaidia sana mfano mifugo ni lishe kwa wanafunzi na kuiuza kupata
fedha ili kuendesha shule.
Mh.Mpogoro alianza kwa kuwapongeza
wajumbe wa bodi ,mwalimu mkuu ,walimu na uongozi wa serikali kwa namna
wanavyoshirikiana na shule hyo .
Mh Mpogoro amewaambia wajumbe wa
bodi hyo kuendelee kuisimamia shule hyo kwani inatoa huduma kwa watanzania
swala la elimu sio mali ya ccm ,elimu ni maslahi ya jamii nzima na hivyo
kuwataka wajumbe wa bodi kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanaleta watoto
masimbwe na kuachana na wanasiasa uchwara wanaopinga maendeleo ya shule
hiyo .
"ni kweli shule hyo ni mali ya
jumuiya ya wazazi lkn elimu sio mali ya jumuiya hyo.
Hivyo amepinga vikali wapotoshaji na
amewaomba walimu wa ufundi kuhakikisha vijana wanaiva ili watokapo hapo wawe
mafundi wazuri na kujikwamua haswaa katika swala zima la uchumi,kada zote
umeme,ushonaji,ufugaji wa samaki na kuku kuhakikisha wanatoka hapo kwenda
kujitegemea na vilevile waweze kuhakikisha wanafunzi wanaosoma masomo ya
kawaida kidato cha kwanza na nne kuhakikisha wanafaulu vyema ili kuweza
kuitangaza shule hiyo.
Mh mpogoro ameahidi kwa nafasi yake atashirikiana na
wadau mbalimbali kuhakikisha changamoto zinazoikabili shule hyo
zinatatuliwa kwani wazazi mkoa wa Njombe wamewekeza zaidi imani kwake hivyo
hanabudi kuitumikia jumuiya hyo kwa nguvu zake zote.
Naye mtendaji mkuu wa jumuiya ya
wazazi mkoa wa Njombe ndugu Lucas Nyanda ameweza kumpongeza mwkt wake kwa
kufika shulen hapo ,pia wajumbe wabodi na uongozi wa shule pamoja na walimu kwa
jitihada kubwa wanazozifanya kuhakikisha shule hyo inasonga na kuzidi kutoa
huduma kwa watanzania.
Ndugu Nyanda amesema wao kama chama changamoto ndogondogo hazikosekan
na kwa nafasi zao watazisimamia kuhakikisha zinatatuliwa ili shule izidi kutoa
elimu bora kwa watanzania,amewaomba wajumbe wa bodi kuwa wajumbe wazuri na
mabalozi wazuri katika kuhakikisha wazazi,wanawaleta watoto wao shuleni hapo.
Naye mwkt wa bodi ya shule Iginasi
Mkechi,amepongeza ujio wa mwkt kwani anaamn watazd kushirikiana zaidi katika
kuhakikisha shule inasonga mbele na wao kama wajumbe wa bodi watahakikisha
mambo yote yanakwenda sawa na hivyo kuwataka wazazi kuleta watoto wao pale
kwani watapata elimu ya kawaida na elimu ya stadi za kazi ambayo itawafanya
wawe na uwezo wa kujitegemea baada ya kumaliza masomo yao
Tazama zaidi Picha Hapa Chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni