MWENYEKITI WA WAZAZI-CCM MKOA WA NJOMBE NA TIMU YAKE WAKUTANA NA DC, WAKUU WA IDARA HALMASHAURI YA W/LUDEWA, ATEMBELEA SHULE YA WAZAZI SEKONDARI YA LUDEWA NA KUACHA NEEMA KWA SHULE ZOTE MBILI.
Na Stambuli Titho.
Milima
ya Ludewa imezidi kupasuka na kuacha maji ya kitoka kwa wingi Baada ya
kigogo wa ccm kufanya ziara wilayani humo na kuhakikisha ccm inaisimamia
serikali kwa maslahi ya wananchi.
Huu ni
mwendelezo wa ziara ya mwkt wa wazazi mkoa wa Njombe Ndugu Josephat
Mpogoro na katibu wa wazazi mkoa wa Njombe -Lucas Nyanda ,wakiwa
wameambatana na mjumbe wa kamati ya utekelezaji wazazi mkoa mhe mgina na
uongozi wa ccm, jumuiya ya wazazi ludewa.
Ambao
leo 19/07/2018,amewasili ofisi za DC na kukutana na Mh Mkuu wa wilaya
Andrea Tsere na wakuu wa Idara wa Halmashauri ya W-ludewa.
Baada
ya utambulisho mwkt aliweza kupata taarifa ya kiutendaji ya hamlashauri
kutoka kwa wakuu wa idara wakiongozwa na DC,Hasa Afya, elimu na
maendeleo ya jamii.
Upande wa Afya Mh DC amemueleza
mwkt kuwa serikali Imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kufikisha huduma kwa
karibu na Dawa zinapatikana serikali inajitahidi sana, na mpaka sasa
kuna ujenzi wa vituo vya Afya 15,Hivyo upande wa Afya hali ni shwari na
changamoto ndogondogo zinaendelea kutatuliwa.
Upande
wa Elimu Hali ni nzuri na kila siku wanapambana kuhakikisha wilaya ya
ludewa inakuwa sawa lakin kunachangamoto kubwa katika elimu hasa mimba
mashuleni ambapo mpaka sasa kesi 23,ziko mahakaman na wanahakikisha haki
inapatikana kwa mtoto wa kike, pia utoro mashuleni na Baadhi ya wazazi
kutokuwa na ushirikiano wa kutosha walimu wao kama serikali wanalazimika
kutumia nguvu kubwa kuhakikisha mambo haya yote hayaathiri mfumo wa
elimu.
Upande wa maendeleo ya jamii serikali
kupitia idara hyo imeweza kushiriki vilivyo mkakati wa kupunguza
umaskini wameendelea kutoa mikopo kwa vijana na wanawake na wikimbili
zilizopita wamekabidhi hundi ya shillingi million 20,Changomoto katika
urejeshaji ni hafifu hasa Kwa vijana ,Hivyo amemhakikishia Mh mwkt
mpogoro kuwa wanazd kupambana na masawala ya Miundombinu kama vile
Barabara ,umeme na maji.
Na pia ameweza kumweleza
mwkt kwamba wakulima wa ludewa watakombolewa soko La mahindi kupitia
serikali na taasisi binafsi kupitia AMCOS kwani mahindi ya Ludewa
yameonekana yanakiwango bora na hivyo kuwa kama zao la biashara na
yatauzwa kwa bei nzuri hivyo serikali kuwakomboa wakulima.
Baada
ya kupokea report hyo mwkt ameonekana kuridhishwa na kasi ya mkuu wa
wilaya hyo ya kupambana na changamoto za wananchi hasa katika swala zima
la kuwa komboa wakulima,utoaji mikopo, kuhakikisha miundombinu inakuwa
sawa na kudhibiti changamoto zoto zote zinazoathiri elimu wilayan
ludewa.
Pia amewaomba wakuu wa Idara kuisoma ilani
ya ccm inaeleza nn Juu ya wilaya yao, kazi kubwa ya ccm ni kuhakikisha
watumishi wanatekeleza vyema waliyoyaahidi.
"Hatutakuwa wapole kwa mtumishi yeyote asiye weza kutekeleza vyema Ilani ya ccm"
Kwani ccm inadeni kwa wananchi kwasababu waliahidi wakati wanaomba kura na wananchi waliwaamn.
,Hivyo anawaomba wafuate ilani ya uchaguzi na inasema nini, na kuwahudumia wananchi "uongozi ni utmishi na sio utukufu ".
Baada ya hapo alielekea shule ya sekondari ludewa inayomilikiwa na jumuiya ya wazazi.
Baada ya kuwasili shuleni hapo alilakiwa na mkuu wa shule na mwkt wa bodi ya shule..
Zoezi
la kwanza lilikuwa ni utambulisho wa uongozi wa shule na watumishi wa
shule na msafara wa mwkt, Baada ya hapo mwkt alipata taarifa ya
maendeleo ya shule kutoka kwa mkuu wa shule ambapo katika taarifa yake
ameweza kumweleza mwkt hali ya maendeleo ya shule hiyo ni shwari kwani
kila siku shule huyo imeendelea kufanya vizuri na kuungwa mkono na wadau
,pia shule inajishughulisha na miradii mbalimbali kama vile ufugaji,
ufyatuaji wa tofali, kilimo cha maparachichi na mahindi ambayo inasaidia
kutoa lishe kwa wanafunzi na elimu ya kujitegemea MA biashara ili
kuongeza nguvu ya fedha ya kuendeshea shule.
Baada ya hapo alitembelea miradi ya shule kuona uhai wake.
Baada
ya kutembelea miradi alifanya kikao na wajumbe wa bodi,na walimu
,Amewapongeza walimu kwa jitihada wanazozifanya za kutoa elimu kwa jamii
kwani wanaikomboa jamii kwa kiwango kikubwa, lkn pia bodi ya shule kwa
jitihada kubwa ambazo wanazifanya kuhakikisha mirad na taaluma ya shule
inaimarika yeye kama mwkt anafarijika sana, na anawaombea juhudi hizo
ziendelee ili kuhakikisha watanzania wanapata ukombozi wa elimu.
Lakini pia
amewataka wazazi kupinga vibaya kauli zinazotumiwa na wanasiasa shule
zinazo milikiwa zinatoa elimu ya ccm ,amewataka viongozi hao kupuuza
kauli hizo kwani elimu sio mali ya ccm ila shule inamilikiwa na jumuiya
ya wazazi kwani lengo la wazazi ni kukomboa jamii hivyo walilazimika
kuanzisha shule kwa kutambua wajibu wao.
"wapo
watoto walioshindwa kwenda shule za serikali, wanaotaka kujiendeleza
kimasomo na wapo wanaotaka kurudi shule baada ya kuahirisha masomo kwa
sababu tofautitofauti hivyo shule hizo zimekuwa mkombozi "
Amewaomba
walimu kuwa na moyo wa uzalendo juu ya shule hizo, ameshukuru pia kwa
walimu kuanzisha kilimo cha parachichi, Amempongeza pia katibu mwenezi
ccm mkoa wa Njombe Cde Erasto Ngole kwa kutoa miche 45,na yeye pia
ataunga mkono kwa kutoa miche ya parachichi 100 na ametoa shillingi
50000/=,pia amempongeza Padre aliyejitolea kitanda kwa ajili ya
wanafunzi "nasema ahsante sana"
Pia amewapongeza
wajumbe wa bodi baada ya kuchaguliwa kila mmoja alichangia shillingi
50000/=,"nasema ahsanten Sana Mungu awabariki "
Mtendaji
wa jumuiya hiyo ya wazazi Ndugu Lucas Nyanda amempongeza mwkt wa wazazi
mkoa wa Njombe kwa kutembelea shule hyo kwani ujio wake utasaidia
kuziona changamoto ndogondogo zinazoikabili ili kuweza kushirikiana na
bodi ya shule ili kuweza kuzitatua. Ameonekana kuibebesha mzigo bodi ya
shule kwa kuipa imani 100%,hivyo matumaini makubwa yako kwao kwa
mstakabali wa shule hyo .
Naye mjumbe wa kamati ya
utekelezaji mkoa wa Njombe Ndugu mgina ameonekana kila mara kuwakumbusha
wazazi kuthamn sana elimu kwa kutupia macho shule za wazazi kwani
zimekuwa msaada mkubwa ,ameweza pia kuchangia vitanda viwili double deka
masimbwe kimoja na ludewa kimoja na magodoro yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni