Dstv Tanzania

KATIBU WA WAZAZI-CCM MKOA WA NJOMBE NA MJUMBE WA BARAZA WAZAZI -CCM TAIFA WATIKISA JIMBO LA LUPEMBE WILAYA YA NJOMBE HUKU MBUNGE HONGOLI AKIONYESHA MAAJABU YA JIMBO LAKE


Na, Titho Stambuli.


Huu ni mwendelezo wa ziara ya viongoz wazazi Mkoa wa Njombe, kutembelea kila wilaya yenye lengo la kuimarisha jumuiya hiyo na kuona utekelezaji wa ilani ya ccm.


Viongozi wa ccm -wazazi ngazi ya mkoa Katibu wa wazazi mkoa wa Njombe Cde -Lucas Nyanda akiwa ameambatana na Mjumbe wa baraza kuu wazazi taifa wakiwa Ndugu imani fute wamefanya ziara wilaya ya Njombe ambapo wameanza na Jimbo la Lupembe.


Mapema leo walipowasili wamelakiwa na viongozi wa wilaya hiyo jumuiya ya wazazi Mwkt wazazi wilaya ya Njombe Ndugu kasanga Makweta, Katibu wilaya wazazi Ngogo na wajumbe Pilly mwifunyi na Joyce Gakye   Huku mbunge Jolam Hongoli kwa kutambua umuhimu wa ziara hiyo ameungana na viongozi hao kama kiongozi wa jimbo hilo ili kuwathibitishia utendaji wake wa kazi katika jimbo hilo.

Baada ya kulakiwa jimbon humo viongoz wote waliweza kutembelea shule ya Sekondari Ninga kujionea maendeleo ya shule hiyo ambapo kiongozi huyo ameweza kujionea shughuli nzuri zinavyoendelea shuleni hapo ujenzi wa mabweni, madarasa na Nyumba za walimu ambazo zinajengwa kwa nguvu za wananchi ,serikali na mchango mkubwa kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo Mh Jolam Hongoli,Pia uongozi wa wilaya wazazi umetoa limu moja, mbunge tano, mjumbe wa baraza 20,000/=kwaajili ya kuchangia maendeleo ya shule hyo.


Baada ya hapo msafara wa katibu ulielekea kituo cha Afya ninga na kujionea shughul mbalimbali za kuhudumia wagonjwa kituon hapo ambapo kiongoz huyo ameonekana kuridhishwa na Hali ya kazi kituon hapo Huku akimpongeza mbunge wa jimbo hilo kwa ushiriki mzuri wa maendeleo katika kituo hicho cha Afya.


 Katika mkutano huo amekabidhi sabuni box moja na Mbunge wa jimbo hilo akitoa katon tano,pia amewaomba watumishi kuvumilia hali ya mazingira katika utendaji wao wa kazi serikali bado inaendelea na mchakato wa kuboresha, kupandisha mishahara na madaraja. 

Pia Katibu ameweza kuwahutubia wananchi wa kata ya Ninga, katika hotuba yake ameweza kuwakumbusha wananchi hao kuhakikisha wanaipigania ccm, wanasimamia na kutoa taarifa katika mchakato mzima wa maendeleo katika kata yao.


Katika hatua nyingine amepinga vikali kuanza kuandaa wagombea amewaonya na kutaka kuacha hayo mambo kwani ccm haitafumbia hayo na kuwataka wawaache viongozi waliopo madarakani wafanye kazi,pia amewataka viongozi wa jumuiya kufanya ziara katika maeneo yenye kero za wananchi na kuimarisha chama cha mapinduzi .

"msibweteke tuchape kazi kama awamu ya tano ilivyojipambanua". 


Pia amekemea swala za mimba utotoni na kuwataka wazazi na watendaji wa serikali kutolifumbia macho swala hilo kwani linarudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike na kuwaomba wasibweteke pia swala zima la malezi walee katika maadili mazuri.


Huku mbunge wa jimbo hilo akionekana kung'ara kwa mgeni rasmi huyo pale alipokuwa akipongezwa na wananchi na Huku yeye mwenyewe akifafanua zaidi namna miradi inavyo kwenda hasa umeme na Barabara ,huku swala la umeme akitaka wananchi kuwa na subira kusubiri umeme wa REA na swala la barabara tayar ameshawasiliana na TANROADS na mchakato wa maendeleo katika kata hyo uko sawia.


Naye Mjumbe wa baraza wazaz taifa kutoka mkoa wa Njombe akiwaomba wananchi kuunga mkono juhudi za ccm na serikali yake kwakuwa inadhamira ya kweli na taifa hili ,hivyo haoni sababu ya wanaccm kuanza kugawanyika ama watu kuendelea kuunga mkono upinzani.


Msafara huo ulielekea kata ya Ikuna ambapo wameweza kukutana na wananchama wa jumuiya hiyo hawakuwa na ajenda tofauti zaidi ya kuimarisha jumuiya, kukataza maswala ya kampeni, Elimu na mimba kwa wanafunzi na kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kumsemea mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuleta maendeleo katika jimbo la Lupembe.


Lakini pia wameweza kukagua ujenzi wa zahanati kata ya ikuna ambao wameanza ujenzi wa zahanati kata ya ikuna na kuona msingi uliochimbwa Kwa nguvu za wananchi na wanalengo la kupandisha ukuta kwani mawe wameanda na tofali na wanaomba serikali iwasaidie pale watakapohitaji msaada.

Mimi niko lupembe nimepigwa tafu na jumuiya ya wazazi mkoa wa Njombe na Kada kutoka songwe Ndugu Sadock Mwanda.


Zaidi Tazama Picha hapa Chini.






Hakuna maoni: