MDA YALAANI VIKALI TISHIO LA SHAMBULIZI DHIDI YA MWENYEKITI WAKE CLEMENT SANGA NA USALAMA WA FAMILIA YAKE.
KUTOKA UONGOZI WA MDA
23/07/2018
Ndugu zetu wanamakete pamoja na wadau wa maendeleo ya Makete, poleni na majukumu ya kujenga Taifa na wilaya yetu ya Makete.
Uongozi wa Chama cha Maendeleo Makete (Makete Development Association- MDA) tumesikitishwa na taarifa kuwa mwenyekiti wetu wa MDA Ndugu Clement Sanga ametishiwa usalama wake binafsi na familia yake hali hiyo ikihusishwa na majukumu yake katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa timu ya Yanga.
Akiwa kiongozi wetu katika MDA tunampa pole kwa yaliyotokea, nasi tunampongeza kwa uamuzi aliofanya wa kujiuzuru katika nafasi hiyo ya uongozi katika Timu ya Yanga. Tunamtakia utulivu, subira na amani katika wakati huu wa mpito. Mungu amsimamie na kumzingira nyakati hizi.
Uongozi tunaungana na wanamakete na wadau wengine kumpa pole na kumpongeza kwa maamuzi haya aliyofanya akiwa salama yeye pamoja na familia yake.
Aidha tunampongeza kwa uongozi wake mahiri aliofanya kwa kipindi chote alichoiongoza Klabu ya Yanga kwa kuwa kulikuwa na utulivu na mafanikio makubwa kwa kipindi kirefu. Nasi tunaitakia klabu ya Yanga hali ya utulivu na subira katika wakati huu wa mpito ili ivuke na kuendelea salama.
Tunamuomba Bw. Clement Sanga tuendeleze mapambano ya kuwaleta wanamakete na wadau wengine wa maendeleo pmoja katika kuiletea maendeleo wilaya yetu.
------------
ADV. PHILIPO MAHENGE, MAKAMU MWENYEKITI- MDA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni