Dstv Tanzania

WANANCHI WILAYAN MAKETE WAFURAHIA KAMPENI YA AFYA YANGU FURAHA YANGU.


Na stambuli titho.


Kampeni  Ya furaha yangu Afya yangu, inalengo  lengo la kupima Afya kwa watanzania ili kuweza kuwasaidia watanzania kujua Afya zao.


Kampeni hiyo iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka Mkoani Njombe, Ilibisha hodi wilayani makete kutoa huduma hiyo muhimu katika wilaya ya hiyo, kampeni hiyo imepokelewa vyema na wananchi wa wilaya hiyo jinsia zote wanaume kwa wanawake kwa kutambua umuhimu wa kampeni hiyo itawasaidia wote kujua Afya zao na kuwahi matibabu. 


Wameishukuru serikali na wadau wa kampeni hiyo kwani imelenga huduma mhimu katika jamii kwani itasaidia wananchi wengi kujua Afya zao, kujilinda, na kupata matibabu pindi watakapogundulika na ugonjwa wowote Kama vile UKIMWI, TB, au KISUKARI au magonjwa mengine na yasiyo ya kuambukiza. 

Wakifunguka Baadhi ya wanaume katika mtandao wa stambulinews wamewahamasisha wanaume wenzao kuhakikisha wanajitokeza kupima Afya zao ,kwani ni jambo jema kutambua Afya yako kwani endapo utagundulika utaweza kuwahi matibabu na kujikinga na kuwalinda wengine na itasaidia serikali kufikia malengo ya serikali ya millenium Huku wakitoa lai kwa wanaume kukimbia kwa wanaume na kuwaacha wanawake peke yao, kwani endapo kila mmoja atahamasika kupima tutaweza kuzua vifo visivyo kuwa na ulazima na kutokupoteza nguvu kazi ya taifa bila sababu yoyote ile. 


Upande wa wanawake wilayani makete wameonekana kufurahishwa na kuwahamasisha wanaume wakapime Huku wao wakijitokeza kwa wingi kupima, akiongea na mtandao huu Mwanamke Aida konga amewaomba wanawake wenzake kutumia fursa ya kampeni hiyo, huku akitoa lai wanaume kuacha tabia ya kutokupima Afya kwani itawasaidia kujua Afya zao na kuweza kujikinga na kujilinda na hatimaye kupunguza maambukizi yasio na ulazima, kwani wamekuwa wakigoma kwenda cliniki kupima na wake zao jambo ambalo limekuwa linatishia usalama katika jamii hivyo ni muda mwafaka kuhakikisha wanaitumia fursa hii.

Hakuna maoni: