Dstv Tanzania

MPOGORO AIKUSANYA MAKAMBAKO ,ASEMA JUMUIYA YA WAZAZI INAWAJIBU WA KUHAKIKISHA JAMII IKO SALAMA,ASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI UTENGULE.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi -CCM Mkoa wa Njombe Josephat Mpogoro Akishiriki Ujenzi wa Hostel Kwaajili ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Utengule.
Na,Titho Stambuli

Jumuiya ya wazazi mkoa wa Njombe imezidi kuchanja mbuga kila siku katika kuhakikisha inawafikia wanachama wake katika kuimarisha jumuiya hiyo. 

Msafara wa Mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Njombe Josephat Mpogoro ambaye ameambatana na Mjumbe wa baraza kuu wazazi taifa Ndugu Iman fute na katibu wa jumuiya hiyo Ndugu Lucas Nyanda na kada wa chama cha mapinduzi ,mburudishaji na kindakindaki Rozana Tewele.

Ziara hiyo Leo imefanyika makambako Kata ya Maguvani, na Utengule , ziara hiyo yenye lengo la kuimarisha jumuiya, Mwkt kushukuru kwa kuchaguliwa na kuhakikisha jamii inakuwa salama katika kuhakikisha swala zima la elimu, malezi na uchumi. 

Mwenyekiti  na katibu wake wameamua kuhakikisha jumuiya ya wazazi inasimamia swala zima la malezi kwani mmomonyoko wa maadili unadhoofisha maendeleo ya jamii nakuharibu utamaduni wetu.

Mwenyekiti amewataka wazazi kuvalia njuga swala zima la elimu kwani elimu ndio mkombizi wa jamii nzima kwani ili mtoto awe salama ni lazima asome, hivyo kutofumbia macho swala zima la mimba za watoto mashuleni kwani linadhoofisha elimu kwa mtoto wa kike.

Pia amewataka kuhakikisha kutokuwa nyuma katika swala zima la uchumi kuanzia ngazi ya familia na jumuiya ya wazazi, bila uchumi hakuna jambo litakalo kwenda.

Amewataka wazazi kujishughulisha na kilimo, biashara na viwanda vidogo vidogo ili kuweza kukuza uchumi wao, pia katika jumuiya kuhakikisha jumuiya inajitegemea kiuchumi na kwa kuonyesha mfano ameweza kuchangia katika kata ya maguvani miche ya parachichi. 

Wanachama wa jumuiya hiyo wamemueleza mwkt kata ya maguvani haina ofisi hivyo wao wameanza kujipanga kujenga ofisi wameandaa mawe, matofali na wanasubir kuanza ujenzi na hivyo mwkt ameweza kujitolea Bundle Moja La bati.


Pia ametembelea kata ya utengule na amefika katika shule ya sekondari utengule kuona maendeleo ya shule hiyo,Baada ya kuwasili shuleni hapo amepokea taarifa ya maendeleo ya shule hiyo, ambapo mkuu wa shule amemueleza kuwa hali shuleni hapo ni shwari japo changamoto hazikosekani na baadaye akashiriki kazi za mikono za ujenzi wa hostel na amejionea chakula kilichochangwa na wazazi.


Mpogoro  amewapongeza wazazi kwa kushiriki kuinua kiwango cha elimu kwa kuchangia chakula,kwanza amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya na ya maendeleo na kuwataka kuendelea kushikamana na kuwa wamoja kwani swala la maendeleo haliwez kupatikana panapo mgawanyiko,ambapo taarifa ya kata ya ccm inaeleza kuwa wao na serikali ni kitu kimoja changamoto ni kadi naye mwenyekiti ameahidi kuwasaidia.


Msisitizo aliouweka katika ziara hyo ni elimu ,uchumi malezi na maendeleo, wananchi wa utengule msibweteke na vyama vya upinzani ccm pekee ndio yenye uwezo wa kuleta maendeleo hivyo ni lazima muhakikishe mnakipigania chama cha mapinduzi kiendelee kupata maendeleo.

Mimi ni Balozi wa shule za masimbwe na Ludewa sekondari..... Karibu mwanao aweze kupata elimu ya kawaida na ujasiriamali.

Zaidi Tazama Picha hapa Chini.

 

Hakuna maoni: