MWENYEKITI MDA ASEMA WAMEDHAMIRIA KUIBADIRISHA WILAYA YA MAKETE KUWA MFANO WA KUIGWA,ATOA WITO KWA WAZAWA WA MAKETE KUWEKEZA NYUMBANI.
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA) Clement Sanga
amesema Chama hicho kinatarajiwa kuwa Mkombozi kwa WanaMakete katika kubadili
Maisha ya WanaMakete kwa kuwa hamasasisha wenye uwezo kifedha na kifikra
kuwekeza Wilayani Makete.
Akizungumza na Kitulo fm Mwenyekiti huyo amesema azma ya Chama
hicho ni kubadili uhalisia wa Makete katika kuiendeleza kiuchumi,kijamii na
kielimu kwa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo ikizingatia Serikali
ya awamu ya tano inatekeleza ahadi yake ya kuboresha miundombinu ya Barabara
kwa kiwango cha Lami kutoka Njombe mpaka Makete.
Ameongeza kuwa ili kuyafikia Maendeleo yanayotarajiwa ni
lazima kila MwanaMakete mwenye moyo wa kupenda nyumbani aje awekeze nyumbani
kwanza kuliko kuendelea kuwekeza maeneo mengine ilhali Makete kuna fursa nyingi
za Uwekezaji.
“Wafanyabiashara wengi wakubwa waliowekeza Mbeya,Dar es
salaam,Tunduma na maeneo mengine wanaheshimika sana huko waliko,sasa hawa nao
tunawaomba sana warudi pia kuwekeza kwao hapa nyumbani”
“Kusema kweli hii ni azma ambayo tunataka Makete
tubadilike kwa nini sehemu zingine
wameweza kufanikiwa? Why not us? Why not here? MDA tutalipigania hili kwa nguvu
zote kwanza tunaanza na nyumbani” Ameongeza Sanga
Kwa upekee wake Chama hicho kimeweka Makao Makuu ya Chama
Wilayani hapa huku kikitarajia kuanza kujenga Jengo la Chama Wilayani hapa
kuanzia mwakani 2019.
Wakati huohuo hivi sasa Chama hicho kimeunda Kamati mbili
maalumu(Kamati ya Jamii na Kamati ya Uchumi na fedha) Kamati hizi zitahakikisha
zinajihusisha na kufanya kazi kwa Karibu na Kila MwanaMakete aliyepo ndani na
nje ya Makete katika kuhamisisha uwekezaji ndani ya Wilaya yake.
Chama cha Maendeleo Makete mpaka sasa kinazaidi ya miaka
miwili na wanachama wasiopungua 150.
Chama hicho kinaendelea kupokea wanachama wapya na kujiunga
kwa kiasi kidogo cha Fedha kwa mujibu wa Katiba ya Chama ni shilingi elfu 10 tu
kwa mwaka,hivyo kwa yeyote anayehitaji kujiunga anaweza kuwasiliana na Viongozi
wa Chama hicho ili kuijenga Makete pamoja
Katibu wa MDA- - -0768484715 (Award Mpandilah)
Naibu Katibu MDA- - -0715036902 (Monny Luvanda)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni