UVCCM NJOMBE ,WACHARUKA SWALA LA HAKI ZA WALIMU WALIOHAMISHWA KUTOKA SEKONDARI KWENDA MSINGI MKOA WA NJOMBE WAMTWISHA MZIGO MNEC NA KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE.
Na stambuli titho.
UVCCM
mkoa wa Njombe ,wamezidi kuwa vinara wa kushughulika na kero za
wananchi kila mahali ambapo wamekuwa wakiona mambo hayaendi sawa.
Hivi
karibuni uliibuka mgogoro mkubwa kati ya walimu na mkurugenzi ,uongozi
wa walimu na walimu wakuu ,kutokana na serikali kuamua kuwapunguza
walimu sekondari na kuwapeleka shule za msingi kama mpango wa
kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa wa walimu na wnafunzi katika shule
za msingi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Akiwakilisha Mkoa wa Njombe (MNEC) Fidelis Lumato akizungumza na walimu ambao hawapo pichana. |
Mpango wa serikali ulikuwa mzuri lkn
baadhi ya wakurugenzi na uongozi wa walimu wameshindwa kukidhi matakwa
ya taratibu za haki za uhamisho wa walimu.
Hilo
limeibuka na mgogoro mkoan Njombe pale ambapo mkurugenzi Halmashauri ya
mji,uongozi wa walimu na walimu wakuu kugeuka maadui wa walimu
hao,mkurugenzi ameshindwa kuwapa stahiki zao walimu hao na walimu hao
wameonekana kutafuta suluhu kwa kukimbilia ccm.
Hapo ndipo msuguano
ulipoanza kuibuka viongoz hao wa serikali kuanza kuwakandamiza walimu
hao kwa kuwa wameonekana kuwachanganya wao na siasa jambo ambalo
hawakubaliani nalo ,Huku walimu wakinukuu maneno ya raisi wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wakipaza sauti kuwa mtumishi wa serikali
asiyetambua ccm hamfai katika uongozi wake.
Viongozi hao waliweza
kuwahadaa watendaji hao kwa kushirikiana na uongozi wa CCM kuhakikisha
walimu wanapata haki zao na kuhakikisha wanakuwa na amani na wanaendelea
na kazi ya kulitumikia taifa hasa katika swala zima la kuwafundisha
watoto wetu.
Kada wa Chama cha Mapinduzi Kutoka Songwe Sadock Nyanda akisalimiana na MNEC Fidelis Lumato alipowasili katika ofisi mpya za chama hicho mkoa wa Njombe |
Mgogoro huo mwanzo ulionekana
kutokuzaa matunda kwa watendaji wa serikali kwa kuziba masikio kwa
kuamini kuwa ccm si lolote ,hata maagizo yaliyotolewa na ccm mkurugenzi
kufuta barua za kuwasimamisha kazi walimu hao,barua za onyo na malipo
kwa walimu hao vyote hivyo havijatekelezwa na hivyo kuamin kuwa ccm
haina meno katika hili,lkn pia kutishwa kwa walimu hao kumekuwa kukiwapa
hofu walimu hao wakati wao wanadai haki zao.
Vijana
ni jeshi kubwa hawakukubali kushindwa na kuendelea kula nao sahani moja
mpaka baadhi ya walimu wamelipwa lkn wengine wakinyimwa stahiki zao
bila kuwa na sababu za msingi .
Leo tarehe
21/07/2018 UVCCM wamekutana tena na walimu na kumwalika MNEC aweze
kuongeza nguvu kunusuru hali ya walimu hao ambao wamekuwa na wakati
mgumu katika mgogoro huo ,ambao unahatarisha vibarua vyao na mahusiano
n,uvccm wameweza kumweleza MNEC Fidelis Lumato kwa kuwa hawaoni sababu
ya kuendelea kuteseka ili hali wanategemewa katika kulijenga taifa kwani
taifa limewasomesha kwa malengo ya kulitumikia taifa,wao kama UVCCM
wanaumia walimu hao kuendelea kunyanyasika wanashangaa mkurugenzi
kuendelea kuweka mgogoro na walimu hao.
Pia wamenong'onez MNEC kuwa
upembuzi wa walimu hao umeonekana ni wakibaguzi walimu walioupande wa
ccm ndio wamenyimwa haki zao kwa kuwa wao ni ccm jambo ambalo
limewakwaza UVCCM na kuamua kuitisha kikao hicho na walimu ili kuweza
kusikiliza kilio chao.
Kabla MNEC hajasema lolote
alikaribishwa na msemaji wa ccm mkoa wa Njombe Cde -Erasto Ngole ,ambaye
ameonekana kupinga vikali manyanyaso ya walimu hao na hatakubali kama
kuna walimu wakuu shule za msingi wamekuwa kero kwa walimu hao wakome
kuanzia leo na wakirudia wao kama ccm hawatakubali .
Mh
MNEC ameonekana kusikitishwa na kukerwa na kitendo hicho ,huku
akiwapongeza UVCCM kwa kuwa wakali pale mambo yanapokuwa hayaendi
sawa,Amewaomba walimu kuwa watulivu yeye kama kiongozi hatoubaliana
anaungana na jeshi la UVCCM kuhakikisha mslahi ya walimu hao.
Lakini pia
ametoa lai kwa watumishi wa serikai kuacha unyanyasaji yeye katika
hayuko pamoja nao hasa maafisa elimu ambao wameonekana kutupiwa lawama
kwa kuwahadaa walimu hao kwa kuwabeza walimu hao kuwa ccm sio
lolote,yeye kama kiongozi atahakikisha haki inapatikana bila kuyumbishwa
.
"hatutakubaliana nao kama hawana hela
wasiwanyanyase hata raisi ameagiza kwani walimu hawajakubali kuhama ila
haki zao zipatekane kwani kuna ugumu gani"
Vijana wangu tulieni mimi niko nanyi mpka hakizenu zipatikane.
Viongozi wengine walioshiriki kikao hicho na walimu ni pamoja na Katibu uvccm mkoa -Sure I Mwasanguti ,Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve ,katibu
hamasa na chipukizi mkoa Johson Elly Mgimba ,katibu uvccm wilaya Ya Njombe Dany Muhaza na katibu hamasa wilaya Imani Moyo pamoja na Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Njombe Lucas Nyanda
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa na Wilaya ya Njombe wakiwa na Walimu katika picha ya Pamoja mara baada ya kufanyika Mkutano uliolenga kujadili na kutatua changamoto zinazowakabili. |
Mimi naitwa titho stambuli ninayekuletea habari hizi kutoka makao makuu ya ccm mkoa wa Njombe,pia ni balozi wa shue za wazazi.
Picha zaidi Tazama Hapa Chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni