STAMBULI ATIMKIA JUMUIYA YA WAZAZI CCM -MKOA WA NJOMBE, WAZAZI WAMPOKELEA WILAYANI LUDEWA ,ATEULIWA PIA KUWA BALOZI WA SHULE ZA WAZAZI MKOA WA NJOMBE
Na stambuli Titho.
Ziara
ya mwkt wa wazazi wilaya ya Ludewa imeleta manufaa kwa ccm, na wananchi
kwakuwa wameweza kukagua utekelezaji wa ilani, kuimarisha jumuiya na
ccm hakika jumuiya imefanya kazi kubwa.
Jambo la
kupendeza ni kumpokea mwanachama mpya katika Jumuiya hiyo Cde-Titho
Nicholausi stambuli Mtokoma, ambaye amefurahishwa na namna jumuiya hiyo
inavyofanya kazi nzuri kuhakikisha ccm inakuwa imara,lakini pia namna
ambavyo imejipanga kutoa huduma kama vile swala la elimu wameweza kuwa
na shule ambazo zinasaidia kwa kiwango kikubwa kuelimisha jamii kwani
elimu ndio ukombozi wa jamii.
"nimeguswa sana na elimu itolewayo na shule hizo kwani mwanafunzi akimaliza anaweza kuwa na uwezo wa kujitegemea Hivyo sion sababu ya kutokujiunga na jumuiyaa hii''amesema Mtokoma
Wazazi
kwa pamoja wakiongozwa na wenyeviti wa mkoa-Mpogoro na wilaya-kiowi
,wamempokea kwa mikono miwili na pia wamempa baraka zote za kuwa balozi
wa shule za wazazi mkoa wa Njombe Masimbwe na Ludewa na yeye kwa mikono
miwili amepokea uteuzi huo na zoezi la kwanza ameanza kutangaza shule
hizo ili ziweze kutoa elimu kwa watu mbalimbali.
"Nashukuru
kwa kupewa dhamana hii nitaitumikia vyema nafasi ya balozi wa shule
hizi na hakika zitasonga mbele nashukuru kwa kupokelewa Mungu awabariki
"
Titho
Nicholausi stambuli Mtokoma Tyari ameanza kuzitangaza Shule hizo kama anavyoonekana katika Picha hapa Chini akiwa na baadhi ya Wafunzi wa Shule za Sekondari na Vyuo vya Ufundi
Zaidi Tazama Picha Nyingine hapa Chini akiwa na Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi Ludewa.
Titho Stambuliwa akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi mko wa Njombe na Wilaya ya Ludewa |
Titho Mtokoma akiwa na Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Njombe Ndg Nyanda |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni