MWKT WA WAZAZI MKOA WA NJOMBE AHITIMISHA ZIARA KWA KUONGOZA BARAZA LA JUMUIYA YA WAZAZI- CCM WILAYA YA LUDEWA.
Na Stambuli titho.
Mtikisiko
wa ziara ya Mwkt wa Jumuiya ya wazazi -CCM mkoa wa Njombe Ndugu
Josephat Mpogoro akiwa ameambatana na katibu wake Ndugu Lucas Nyanda,
kada Metron Kimomeko na Afisa kutoka ofisi ya uvccm aliyetimkia jumuiya
ya wazazi.
Ambapo Mh mpogoro na msafara wake wamehitimisha ziara hiyo kwa kuhudhuria baraza la jumuiya ya wazazi -CCM wilayan ludewa.
Ambapo
mwkt ameweza kuhutubia baraza hilo kwanza kabisa alianza kuwashuru
wajumbe kwa mapokezi makubwa na ushiriki wao katika ziara yake,Pia
amewashukuru wajumbe kwa kuweza kumpa imani ya kuwa mwkt wa wazazi mkoa
wa Njombe.
Ziara ya mwkt ilibeba ujumbe kama vile
kushukuru baada ya kuchaguliwa, kuimarisha jumuiya na ccm, kujenga
Njombe mpya, Kuimarisha uchumi wa jumuiya, Elimu na kushiriki mikakati
mikubwa ya kupambana na umaskini.
Hivyo amewataka
wajumbe kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za wazazi katika kuhakikisha
jumuiya hyo inakuwa mkombozi katika jamii nzima.
Hivyo
yeye kama mwkt amewataka wajumbe kutokuwa wanyonge nakutambua kuwa na
wao ni sehemu ya viongozi wenye kuweza kuisaidia serikali ili iweze
kutekekeleza ilani ya ccm kwa maslahi ya taifa hili.
Yeye kama mwkt anawategemea wajumbe katika kuhakikisha jumuiya inakuwa na nguvu.
Huku
katibu wa wazazi mkoa wa Njombe Ndugu Lucas Nyanda ameweza kuwashukuru
wajumbe kwa mapokezi na kuhakikisha ziara ya mwkt inafanikiwa hivyo
mamba mengi wamefanya wanahitaji sana ushirikiano wao na pia watambue
dhamana ya uongozi waliopewa kwani wameaminiwa na jumuiya kuongoza hivyo
anawaomba wawatumikie wananchi .
Naye mjumbe wa
Baraza kuu taifa Ndugu imani fute ambaye hajaambatana na mwkt kwa kuwa
yuko na majukumu mengine ya kikazi, ameweza kupiga simu kwa wajumbe kuwa
atawanunulia wajumbe kadi 50 na kanuni 10,Huku mwkt wake akiongeza
kanuni tano.
Naye mbunge wa Ludewa Mh Deo Ngalawa
amemuhakikishia mwkt kuwa Ludewa ni salama nayeye kwa kushirikiana na
serikali wanaendelea kutekeleza ilani ya ccm kwa nyanja zote Afya,
Elimu, miundombinu na mambo yote yanayosababisha maendeleo ya elimu,.
Ametolea mfano swala la elimu kunashule sita zinaendelea kujengwa,kwa
upande wa Afya pis kunavituoa kumi na saba vinajengwa na mwezi wa
09,wananchi WA ludewa wataungwa umeme grade ya taifa na umeme wa
jenereta na amewaomba wajumbe kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali.
Naye
mwkt wa ccm mzee Kiowi amewashukuru wajumbe kwa kuhudhuria baraza hilo
na pia amemshuruku mwkt wa wazazi kwa kuweza kufanya ziara hiyo kwani
imeweza kuleta neema wilayani ludewa, kwa kuchangia shule za wazazi, na
kuhamasisha maendeleo kwa wananchi,.
Ziara yake imekuwa na tija kwa
wananchi na wanamuomba arudi tena Ludewa kwani wanatamani kuendelea
kuwa naye ludewa katika kuiunga mkono CCM
Zaidi Tazama Picha hapa Chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni