Dstv Tanzania

ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE KUPITIA ACT JIMBO LA NJOMBE KUSINI EMMILIAN MSIGWA ATANGAZA KUACHANA NA SIASA ZA AINA YOYOTE.

Mimi Emilian John Msigwa.

Bila kushawishiwa na mtu yeyote na bila kusikiliza ushauri wa mtu yeyote nautangazia umma wa wananjombe kwa ujumla kuwa kuanzia leo naachana na siasa za aina yeyote na ninabaki kuwa mwanachama tu wa kawaida wa Act. Na kuwa mzalendo wa taifa hili la Tanzania.


Sababu za uamuzi huu ni
 

Kuwa na kazi nyingi binafsi kwa sasa zinazonihitaji kusimamia ili zisonge mbele.

Hata hivyo nitashiriki katika shughuli za kijamii na za kujenga taifa. Zisizoingiliana na siasa au kuhusisha siasa.

Nasisitiza sihami chama na sitahama chama. Ila nitabaki kuwa raia wa kawaida.

Nitafikiria kwa mara nyingine kama niendelee na siasa au niachane siasa baada ya miaka 10 kutoka leo.

Naomba radhi kwa wote ambao nimewakwaza kwa namna moja au nyingine.

Emilian John Msigwa
Dsm

Hakuna maoni: