COMRADE AWARD MPANDILA AMPONGEZA DIWANI WA KATA YA ISAPULANO KWA KUIBUKA MSHINDI,AAHIDI KUMPA USHIRIKIANO WA KARIBU
![]() |
Comrade Award Mpandila Kushoto akimpongeza diwani wa kata ya Isapulano Ndg Alphonce Mbilinyi. |
Anaandika Comrade Award Mpandila
Ni siku kadhaa zimepita tangu uchaguzi Mdogo wa udiwani kata
ya Isapulano ufanyike
Katika mchakato mzima nilikuwa Jirani nikifuatilia namna
ambavyo mchakato wa kampeni mzima ulivyo kuwa ukiendelea
Nawapongeza wanaisapulano kwakufuatilia mikutano hiyo
takribani mwezi mzima
Imani Yangu maamuzi yao ya kumpata diwani yametokana na sera
walizosikiliza kutoka pande zote mbili
Aidha naamini wamejionea namna sera za chama cha mapinduzi
kwa maamuzi yao wameamuua kuunga Mkono na kumuchagua ndugu yangu Mpambanaji
kaka ALPHONCE MBILINYI
Niwashukuru viongozi wangu wa chama kutoka ngazi ya Taifa ,Mkoa,Wilaya
na Matawi
Mumeonyesha ushirikiano wa hali ya juu saana ushindi
tuliopata ni ushindi wa kishindo
Nakupongeza Mh Diwani kaka ALPHONCE nikiwa mwanachama hai wa chama cha mapinduzi
na mzawa wa kata ya Isapulano tutaendelea kukupa ushirikiano wa hali ya juu
kabisa
Mwisho niwashukuru wazazi wangu kaka zangu wadogo zangu
Binamu zangu kutoka kata ya Isapulano kwa uchaguzi huu niwaombe tuunganishe
nguvu ya pamoja tuijenge kata Yetu kwa kushirikiana na kiongozi Wetu tulie
mchagua
#comrade Mpandila Award
#mzawa kata ya Isapulano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni