ATCL Yazindua Safari Yake Ya Kwanza Ya Dar es Salaam Kwenda Bujumbura
Shirika
la ndege Tanzania (ATCL), jana Agosti 30, 2018 limeanza safari yake ya
pili ya nje ya nchi ikielekea Bujumbura, Burundi.
Safari hiyo ilianza jana asubuhi saa 3 kamili ambapo ndege aina ya Bombadier Q400, iling’oa nanga uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Dar es Saalam.
Taarifa
iliyotolewa Agosti 30 na Kitengo cha Habari na Maelezo cha Waziri
Mkuu, imeeleza kuwa hiyo inakuwa ni safari ya pili ya nje ya nchi baada
ya ile ya Agosti 26 ambapo ndege hiyo ilielekea Entebe, Uganda.
“Kuanza
kwa safari hiyo mpya ya Bujumbura kutafungua milango ya kibiashara na
kitalii baina ya Tanzania na Burundi, pia kutaongeza wigo wa safari za
ndege za shirika hilo linalofufuliwa,” imesema taarifa hiyo
Akipokea
ndege kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreaamliner, Julai mwaka huu, Rais
John Magufuli alisema nchi inang’aa na imefunguka kimataifa kwani
uwezo upo na nia ya kuona shirika la ndege la Tanzania linaimairika,
nayo ipo.
Alilitaka
shirika hilo kubuni mikakati ya kibiashara ambayo itawawezesha kudumu
kwenye ushindani lakini pia kupata faida ya kutosha na hatimaye kutoa
gawio kwa serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni