Dstv Tanzania

KONGAMANO LA MAADILI WAZAZI W-YA WANGING'OMBE LATOA MAJIBU KWANINI MAADILI YANAMOMONYOKA.

Wa Kwanza Kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole Kulia ni Katibu Mpya wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wanging'ombe Agness Kassela Wakiwa katika Kongamano la Maadili Wilaya ya Wanging'ombe.
Na.Titho Stambuli.
Kongamano la maadili la wazazi wilaya ya Wanging'ombe limetoa taswira mpya juu ya maadili,Katika kongamano hilo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Ndg Erasto Ngole (shikamooparachichi).
Kongamano hilo limeandaliwa na Katibu wa  jumuiya ya wazazi  wilaya ya Wanging'ngombe Ndg Juma Nambaila, kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na binafsi(NADO), shule na walimu pamoja na mkuu wa wilaya ,na chama cha mapinduzi wakiongozwa na mwkt wa ccm wilaya ya Wanging'ombe Ndg Kinyangadzi. 
Wa Pili Kulia aliyevaa Shati la Kijani ni Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Comrade Brother Ally Kasinge.
Ujumbe wa kongamano hilo lilikuwa limebeba ujumbe wa maadili(mmomonyoka wa maadili na tunaweza vipi kuhakikisha maadili yanakuwa sawa kwa taifa letu na jamii kwa ujumla).
Akihutubia katika kongamano hilo mgeni rasmi Ndugu Erasto Ngole Amesema"wazazi tunajukumu kubwa kuhakikisha watoto wetu wanakuwa na maadili mema kwa usalama wa taifa letu"
Katibu Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Wanging'ombe  juma nambaila
Amewataka wazazi kukemea mienendo mibaya pale tunapoona watoto wetu wanayumba, bila maadili hakuna tutakacho fanya kwakuwa mambo mengi yanahitaji nidhamu na uhakika elimu inahitai nidhamu, uchumi unahitaji nidhamu na kufanikiwa kunahitaji nidhamu bila hivyo hakuna kitakacho fanyika.
Mwenye Suti ya Bluu ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi Mkoa wa Njombe Ell Johnson Mgimba
Akizungumza na mtandao huu katibu wa wazazi wa wilaya hiyo suluhu ya kupotea kwa maadili ni wazazi kukaa chini na kuwakanya watoto ni lazima kwanza wazazi wakae chini bila kujali umri wa mtoto wake, pia watoe elimu watoto waweze kutambua madhara ya kupotoka kimaadili.

Hakuna maoni: