Dstv Tanzania

CCM MAKETE WAFUNGA KAMPENI KATA YA ISAPULANO TAYAR KWA UCHAGUZI KESHO TAR 12/08/2018.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Makete ONA NKWAMA akiserebuka kabla ya kuanza kwa mkutano  wa kufunga Kampeni za Kumnadi mgombea wa udiwani kata ya Isapulano Alphonce Mbilinyi

Chama cha mapinduzi wilaya ya makete wamefunga kampeni za uchaguzi mdogo za udiwani kata ya Isapulano. 


Viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya zake zote wamekusanyika kwa ajili ya kuungana na viongozi wa wilaya ya makete kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwan kata ya Isapulano.
Katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiwa katika Kampeni za Lala Salama wilayani Makete
Viongozi ngazi ya mkoa wakiongozwa na Mwkt wa mkoa Mzee Jassery Mwamala, katibu mkoa Hosea Mpagike katibu mwenezi Erasto Ngole , Mwkt Uvccm Nehemia Tweve na Katibu Sure Mwasanguti na Katibu Hamasa Johnson Mgimba, Upande wa wilaya ya Njombe ukiwakilishwa na Antony Katani na wanging'ombe ukiwakilishwa na Mwkt Uvccm wilaya hiyo maiko vidoka.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti akipigilia Msumari kuhakikisha CCM Inashinda kwa Kishindo hapo Kesho.
Huku viongozi wenyeji wakiongozwa na Mwkt wao ONA NKWAMA, Katibu wake Langael Akyoo na mjumbe wa kamati ya siasa Joyce sigalla.


Kila kiongozi kwa wakati wake amelitumia jukwaa kuweza kuelezea mafanikio ya Serikali awamu ya tano hasa wilaya ya makete na kata ya Isapulano kwa uwajibikaji wa Serikali upande wa Afya, Elimu, Maji, barabara na usalama ndani ya kata hyo .
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh.Christopher Ole Sendeka akisalimiana na moja ya Kiongozi wa CCM
Hivyo wamewaomba viongozi wa Kata hiyo na wananchi kuweza kumuunga mkono mgombea huyo Alphonce Mbilinyi kwa kuwa wanauhakika kasi ya maendeleo itakuwa kubwa kwa kuwa atakuwa ameingia kutekeleza ilani ya ccm ambayo ndiyo inatekelezwa.
Katibu  wa CCM Wilaya ya Makete   Langael Akyo
RC wa Njombe naye amehutubia jukwaa kuwahakikishia usalama wananchi hao akitaka wananchi kujitokeza na kutumia haki yao ya kikatiba,kwakuwa Serikali imejipanga kuhakikisha usalama upo.
Katibu Hamasa na chipukizi mkoa wa Njombe Johnson Mgimba
Tukutane kumchagua Alphonce kesho.

Zaidi Tazama Picha hizi hapa Chini.
Katibu wa Hamasa Johnson Mgimba akiserebuka
Mbunge wa Jimbo la Makete Prf.Norman Sigalla (kulia)akiteta jambo na katibu wa UVVCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti wakiwa na mwananchi.
Mwenyekiti UVCCM Wilaya ya Wanging'ombe Gombe Michael Vidogo
Kada Mahiri wa Chama cha Mapinduzi Robert Shejamabu hakuwa Nyuma kuhakika hapo Kesho kinaeleweka.
Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Erasto Ngole Wakiserebuka kushoto ni Katibu wa Hamasa na Chipukizi mkoa wa Njombe Johnson Mgimba.
Katibu wa CCM Mkoa wa  NJombe Hosea Mpagike
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Hehemia Tweve

Hakuna maoni: