Dstv Tanzania

MWENYEKITI WA CCM MKOA -NJOMBE AMNADI MGOMBEA UDIWANI CCM KATA YA ISAPULANO -MAKETE

Mwenyekiti wa ccm mkoa wanjombe Cde -Jassery mwamwala akimnadi mgombea wa udiwani kata ya isapulano Alphonce Mbilinyi
Mwenyekiti wa ccm mkoa wanjombe Cde -Jassery mwamwala amefika wilayani makete kuongeza nguvu kumnadi mgombea wa CCM Alphonce mbilinyi, ili kujihakikishia ushindi wa kishindo kwa mgombea wa ccm.

Mkutano huo ulifurika mamia ya wananchi waliofika kudhihirisha wanamahaba na mgombea wa CCM

Mwenyekiti huyo ameambatana na viongozi Wengine ngazi ya mkoa Mwkt Uvccm -Nehemia Tweve na Katibu Sure Mwasanguti. 
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti akimnadi mgombea wa Udiwani kata ya Isapulano
Akiwahutubia wananchi wa kata ya Isapulano waliokusanyika kumsikiliza, amewaomba kukiamini chama cha mapinduzi kwani mambo mengi yanafanyika kwa maslahi ya uma kama vile maji, umeme, elimu na afya, hivyo wamchague diwani ambaye atasimamia ilani ya CCM si mwingine ni Alhponce mbilinyi ambaye ataweza kuwasidia kwa kuwa ilani ya inayotekelezwa na Serikali ni ya ccm, hivyo kumchagua Diwan wa upinzani atajiuzulu tena na kujiunga na ccm hivyo ni kupoteza muda.
 Tazama picha zaidi
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve akisalimiana na wananachi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Kumnadi Mgombea Udiwani kata ya Isapulano.


Hakuna maoni: