DC HOMERA ACHANGIA MIFUKO 50 KWA AJILI YA UJENZI WA OFISI YA CHAMA CHA WAZEE NA WASTAAFU TUNDURU(CHAWATU) NA AAHIDI KUWA UNGA MKONO MPAKA UKAMILISHAJI WA UJENZI HUO.

* Awaomba Wazee waendele kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
* Aelezea azma ya kuanzisha Tamasha la ngoma za Asili Tunduru.
* Awaelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani Tunduru.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera leo 12/8/2018 amekutana na wazee ambao ni wanachama wa Chama Cha wazee na Wastaafu Tunduru(CHAWATU), kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa krasta wilayani Tunduru.
Akifungua kikao hicho Makamu Mwenyekiti Ndugu Selemani Abdallah, alielezea changamoto wanazokutana nazo wazee na wastaafu wilayani Tunduru, ambapo pamoja na mambo mengine aliipongeza serikali kwa kuwezesha wazee wa Tunduru kupata vitambulisho vya kutibiwa bure hivyo wanaishukuru sana Serikali ya CCM ya awamu ya 5.
Alimuomba Mhe. Homera aweze kuwasaidia ujenzi wa Ofisi yao ili waweze kuratibu shughuli zao za kila siku ikiwemo usimamiaji wa miradi yao waliyoibua na inayoendelea kukua kila siku na pia alishukuru Idara ya ardhi kwa kuwapa kiwanja cha kujengea ofisi na Mbunge wa Tunduru Kaskazini Mhe. Ramo Makani kwa kuchangia bati 50 na Tsh 5,000,000/= Kwaajili ya ununuzi wa shamba la mikorosho na kiwanja hicho.
Aliongeza kuwa wazee ni kama wamesuswa kwa sasa ila alimshukuru Dc Homera kwa kuendelea kuwapa matumaini na kila wanapokuwa na jambo lao hajawai kuwaangusha.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mhe. Homera alianza kwa kuwaomba wazee hao waendele kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ili aendelee kuongoza vyema Taifa letu na pili alimpongeza Kaimu Mkurugezi Bw. Chiza Marando na Mganga Mkuu wa wilaya Dk. Wendy Robert kwa kuwezesha wazee kupata vitambulisho vya kutibiwa bure ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Lakini aliwashauri wazee hao wawe na tabia ya kurejesha, mrejesho wa taarifa za miradi yao wanayoitekeleza na wakiwa na changamoto yeyote wasisite kwenda ofisini kwake muda wowote.
Aliwaeleza kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya 5, Tunduru inakuwa kwa kasi sana kila kukicha miradi ya maendeleo inaendelea kuja na miundombinu inazidi kuboreshwa.
Kwenye sekta ya Elimu hadi sasa Chuo Kikuu Huria kimefungua tawi lake (Coordination centre) na wanafunzi wapo wanaosoma Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili, hata hivyo katika kutatua changamoto ya miundombinu ya Elimu imetatuliwa kupitia mfuko wa Elimu, madarasa zaidi ya 150 yamejengwa, madarasa zaidi ya 70 ya nyasi yamejengwa na yameezekwa bati na nyumba zaidi ya 5 za walimu zimekarabatiwa. Zaidi ya Bilioni 1.58 zimetumika kwenye sekta ya Elimu, ujenzi wa Maabara katika shule za sekondari, wanafunzi zaidi 36 ambao ni walemavu wa ngozi wameweza kupata mafuta ya kuzuia miyale ya jua pamoja na miwani, wanafunzi 5 wenye ulemavu wa viungo wamegawiwa baiskeli ya miguu 3. Chuo kikuu cha sokoine Morogoro SUA kinatarajia kuanzisha Tawi lake wilayani Tunduru, aliwaambia wilaya imepokea zaidi ya walimu 70 na Waratibu wa Elimu kata zote 39 wamepata pikipiki kutoka serikali kuu Tamisemi kwa kushirikiana na wizara ya Elimu.

Kwenye idara ya Afya, alieleza wilaya imepokea madaktari MD 4, wauguzi na watumishi mbalimbali sekta ya Afya 86 na wote wameripoti kazini na hivi sasa wanaendelea na majukumu yao, Rais Magufuli ametoa zaidi ya bilioni 1.3 kwa ajili ya vituo vitatu vya Afya Mkasale, Matemanga, Mchoteka na hata hivyo malengo ya serikali kituo cha Afya Juma Homera kinatarajiwa kuwa Hospitali ya Mji mdogo na kwa sasa kipo chini ya Halmashauri ya wilaya Tunduru, Dawa kutoka Medical Store Department (MSD) kwa sasa zinafika kwa wakati Vijijini.
Kwenye miradi ya Maji alieleza zaidi ya milioni 300 zimetumika ujenzi wa mradi wa maji ambao umekamilika Nanjoka na kwa baadhi ya vijiji na Mchangani nk mradi mpya wa maji nakayaya na mgomba nk unatarajiwa kutekelezwa wakati wowote kuanzia sasa zaidi ya milioni 300 kutumika na zaidi ya visima 60 vimechimbwa katika vijiji vyenye matatizo ya maji na bado zoezi la kuchimba visima linaendelea ili wananchi wapate maji safi na salama.
Alielezea mpango wa ujenzi wa Kiwanda cha Korosho Tunduru ambacho kitakuwa kubwa kuliko vyote katika ukandwa wa Afrika Mashariki, kwa sasa Ghala la Korosho la bilioni 5.7 linaendelea kujengwa, Suma JKT nao wanaendelea kusafisha maeneo yao ambapo wanategemea kuanzisha shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo viwanda vidogo vya kati vya korosho, Alisisitiza wazee waendelee kuwa na imani na serikali kwa kuwa viongozi wa vyama vya msingi walioiba fedha za wananchi wamerejesha fedha hata wale waliojiteka walirejesha fedha zote na safari hii kwenye malipo benki ya Crdb pamoja na Nmb watakuwa na mobile bank kwa ajili kulipa wakulima hivyo wananchi hawatakuwa na usumbufu wa kusafiri hadi Tunduru Mjini.
Kwenye sekta ya Utalii alielezea juhudi zinazofanywa na Serikali ya kuendelea kuitangaza Tunduru na kwa sasa operesheni ya kuzuia ujangili pamoja na matukio ya tembo yamepungua, alielezea juhudi za Mwekezaji wa Luxury Safari ambae amewekeza huko Nalika na mwisho alielezea azma yake ya kuanzisha Tamasha la ngoma za Asili ili kutunza na kulinda mila na desturi ya kiyao.
Mwisho Dc Homera aliwaeleza dhamira ya kujenga stendi ya Mabasi ya kisasa na fedha zitakazo tumika kwenye ujenzi huo ni ufadhili toka wizara ya Fedha/Serikali Kuu chini ya miradi ya kimkakati ya kuongezea mapato Halmashauri inayotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi, ambapo eneo lenye ukubwa wa hekari 15 limeshatengwa Nakayaya, Shilingi milioni 32 toka mapato ya ndani zimeshatumika kwa ajili ya kusafisha eneo hilo. Stendi hio itakuwa na uwezo wa kuingiza Mabasi makubwa, Mabasi ya kati, teksi, bajaji, bodaboda pamoja na magari binafsi kwa ajili ya kusindikiza wasafiri na kutakuwa na jengo la utawala, eneo la kupumzikia wasafiri, Choo, mgahawa, ofisi za kukatia tiketi, gereji, fremu za maduka na miundombinu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.
#TUKUTANESITE
#HAPAKAZITU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni