Dstv Tanzania

KATIBU MWENEZI MKOA WA NJOMBE AICHANGIA KWAYA YA MT. SESILIA SH. 1,000,000/=,KIGANGO CHA IDOMAGE -ITULIKE.

Cde Erasto Ngole ambaye ni Katibu mwenezi CCM mkoa wa Njombe

Na Titho Stambuli.


Cde Erasto Ngole ambaye ni Katibu mwenezi CCM mkoa wa Njombe, amezidi kuonyesha mapenzi yake kwa wananjombe kwa kutaman kila mmoja, ama kikundi wafanikiwe. 

Tarehe 08/08/2018 alibisha hodi kanisani idomage -Itulike Licha ya kumuomba Mungu ilimpendeza kurudishia fadhila mwenyezi Mungu kwa kumjalia roho ya kutoa na upendo na pia kufanikiwa katika KILIMO cha Parachichi.


Bingwa huyo wa siasa ameweza kuchangia shillingi 1000,000/ kwaajili ya ununuzi wa sare kwaya ya mtakatifu sesilia inayohudumu kanisani hapo ambapo yeye mwenyewe anasali kanisani hapo.


Akihojiwa kwann amekuwa mtu wa kujitolea sana hatukuweza kupata majibu na akisema kwamba hapa ni kanisani kila mmoja anatakiwa kutoa sadaka kadri Mwenyezi Mungu alivyomjalia. 


"hapa mimi nimekuja kama muumini mwingine na nimetoa sadaka yangu kadri Mwenyezi Mungu alivyonijalia, natoa wito hata ukiwa na mia tano changia neno la Mungu liweze kuwafikia watu wengi " 


Katibu huyo Mwenye uwezo pia wa kuimba na amekuwa akifanya hivyo kwakuwa ni wajibu wa kila muumini kutumia talanta yake kumsifu muumba wake,amesema pia akiwa kwenye siasa atazamwe kama mwanasiasa na akiwa kanisani atazamwe kama muumini Mwingine.


"niwaombe watu wote wawe wanakumbuka kusali na kufanya matendo mema kila wakat kwani hayo ndiyo mambo yanayo mpendeza Mungu, na sio kuja kanisani halafu unamatendo mabaya ,hujitolei na unamaadui wengi"

Lakini pia amewaomba watu kujifunza kusamehe na kusaidia wasiojiweza hayo ndiyo tunayoagizwa na Mungu na hiyo ndiyo dini ya kweli kupiga Magoti kila siku haitoshi.

Hakuna maoni: