Dstv Tanzania

KATIBU MWENEZI MKOA WA NJOMBE ACHANGIA shillingi 300,000/= UJENZI WA SHULE YA MSINGI LUVULUNGE -MAKETE.

Katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Cde -Erasto Ngole
Na Titho Stambuli.

Hakuna Shaka juu ya roho nyeupe na ya upendo ya katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Cde -Erasto Ngole katika swala zima la maendeleo mkoa wa Njombe. 

Siasa yake haijatenga wala kugawa watu katika maendeleo. 


Akiwa katika shuguli zake za kueneza kilimo cha parachichi kwa watu na taasisi alifika katika shule ya msingi Luvulunge wilayani makete na kukuta shughuli ya ujenzi inaendelea yeye kama mdau wa maendeleo na elimu aliweza kuunga mkono juhudi hizo kwa kuunga mkono kwa kuchangia shillingi 300,000/= kwaajili ya ununuzi wa saruji katika kuchangia ujenzi wa shule hiyo.


"Furaha yangu ni kuona maendeleo ya jamii zetu yanakwenda mimi kama kiongozi ninatakiwa kuwa mbele zaidi na lazima niwe wa mfano natoa wito hata kwa watu wengine kuja kusaidia kuhakikisha maendeleo ya Elimu yanakua "

Ndugu zangu hakuna taifa lolote litakaloendelea bila elimu, Elimu ndio mkombozi wa jamii zetu lazima tuandae mazingira wezeshi ya kuhakikisha tunafika mbali kitaaluma hasa wanufaika ambao ni vijana wetu ili baadaye waje watusaidie na tufike mbali, maana watakuwa na uwezo wa kusimamaia na kuzalisha rasilimali zetu tutapata mainjinia, daktari, na mafundi umeme na fani nyingi unazofanya maisha yetu yasonge huu ndio ukombozi wetu na tutaondokana na ukoloni mamboleo

Hakuna maoni: