KATIBU CCM NJOMBE AWAONGOZA WAJUMBE WA KAMATI YA SIASA W-NJOMBE KUSHUHUDIA MAKABIDHIANO YA MRADI WA MAJI WANANCHI WA MTAA WA PERUHANDA NA SERIKALI-NJOMBE IKIWA NI UKAMILISHWAJI WA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.
Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Antony Katani akiwasha Bomba la Maji Kukamilisha makabidhiano ya Mradi huo wa maji |
Katibu wa CCM mtulivu ndani ya wilaya ya Njombe Cde-Antony katani leo amewaongoza wajumbe wa kamati ya siasa kushudia Serikali ya halmashauri ya mji wa Njombe ikikabidhi mradi wa maji uliokamilika kwa wananchi wa mtaa wa peruhanda tayar kwa kuanza kutoa huduma.
Wao kama CCM wameonekana kuridhishwa na namna ambavyo mradi huo umekamilika kwa kuwa tayar wameshatoa huduma kwa ukaribu kwa wananchi wao kwa kuwa waliahidi kuleta maendeleo wakati wanaomba kura .
Akizungumza na mtandao huu katibu huyo amesema kazi kubwa ya CCM ni kuisimamia serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote kwa ukaribu maji na huduma nyingine.
"Mitaa ya peruhanda na makula ilikuwa na shida ya maji na Leo tumewakomboa wananchi hawa hasa wanawake ni sawa na kumtua ndoo mwanamke kichwan kwakuwa hili tatizo limekuwa likisumbua sana wanawake kwakuwa wamekuwa wakiwajibika mara kwa mara kutafuta maji na leo tumemkomboa mwanamke na familia"
Hata hivyo amewaomba wananchi wa peruhanda waendelee kukiamini chama cha mapinduzi kwa kuwa dhamira yake kubwa ni kuwaletea wananchi maendeleo.
"tunaamn maji yatachangia kukua kwa uchumi ndani ya mitaa hii ,bila maji hakuna jambo kitakalo kwenda hivyo nawaomba wananchi watunze mradi huu kwa kuwa unamanufaa kwao kwaujumla na hakika Afya pia inahitaji maji hivyo ni mhimu CCM na Serikali tukitekeleza wenzetu watunze."
"wanawake wamekuwa wakihangaika kutafuta maji kwa umbali mrefu kupitia hili wanawake watapumzika kutafuta maji kwa umbali mrefu sasa watapumzika "
Ndoa zimekuwa zikiharibika sababu ya kutafuta maji kwa umbali mrefu, sisi tunafurahia sasa tumesogeza huduma karibu.
Zaidi Taza,ma Picha Hapa Chini.
Add caption |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni