KIKUNDI CHA OKOA MAZINGIRA CHAANZISHA PROGRAM YA KUTENGENEZA MKAA MBADALA ILI KUPUNGUZA UKATAJI OVYO WA MISITU MKOANI IRINGA.
Mwenyekiti wa Kikundi cha OKOA MAZINGIRA Ngusa Benjamin |
Kikundi cha OKOA
MAZINGIRA Kilichopo Mkoani Iringa
kimeanzisha Program Mpya ya kutengeneza Mkaa mbadala kwa lengo la kupunguza na kukomesha ukataji ovyo wa
misitu Mkoani wa IRINGA.
Akizungumza na StambuliNews Mwenyekiti wa Kikundi Hicho Ngusa
Benjamin amesema Mpango wa kuanzisha Program Hiyo utasaidia kutunza Mazingira
kwani moja ya marighafi zitumikazo
kutengenezea mkaa huo ni takataka kavu.
Benjamin amesema Kikundi
kinatarajia kuanza kupokea majina ya
wataohitaji kuungana na kikundi hicho kuanzia
tar 16- 08- 2018.
Kauli mbiu ya Program Hii ni " tunza Mazingira kwa
kizazi cha sasa na kijacho "
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni