RC RUVUMA AKAGUA VITUO VYA MPAKA WA NCHI YA TANZANIA NA MSUMBIJI.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Bibi Christina Mndema ,kuanzia tarehe 8-9/8/2018 amefanya ziara Wilayani Tunduru ya kukagua hali ya Usalama katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji katika vituo vya mpakani vya Makande na Wenje.
Katika ukaguzi huo,Mhe.Mndeme amesema ardhi ya Tanzania pamoja na maliasili nyingine za Taifa zetu zinatakiwa kulindwa kwa hali na mali ili kuhakikisha zinakuwa na manufaa kwa wananchi na Uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka watendaji na wananchi waliopo katika vijiji vyote vya mpakani kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi mbili na kuwakumbusha kuwa mpaka huu ni wa kihistoria kwa sababu umechangia kupatikana kwa uhuru wa Nchi ya Msumbiji.
Pia ameagiza kuwa masuala ya ulinzi na Usalama wa mpaka huu yawe ni agenda ya kudumu katika vikao vya vijiji ambavyo vitasaidia kuwatambua wageni ambao wanaingia nchini bila vibali na wananchi kutoa taarifa waonapo viashiria vinavyoweza kuvunja amani.
"Nchi yangu Usalama Wangu"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni