Dstv Tanzania

MWENYEKITI CHADEMA NJOMBE FACKII LULANDALA AJIUNGA NA CCM,AFICHUA UOZO WOTE ULIOPO CHADEMA



Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike,Fackii Lulandala aliyejiunga na CCM katikati na Katibu  Mwenezi Erasto Ngole
Na.Erasto Mgeni.

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Mkoa wa Njombe Fackii Lulandala na makada wengine watatu wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini wamejivua uwanachama na kujiunga na chama cha mapinduzi kwa madai ya kwamba wameridhishwa na utendaji wa serikali iliyopo madarakani.

Makada wengine ambao wameambatana na mwenyekiti huyo ni Edger Msigwa,Lukasi Payovela na Paulo Zakaria ambao wanasema wamechukua maamuzi ya kurejea chama tawala walikokuwa awali baada ya kuona mambo mengi yaliokuwa yakipigiwa kelele na vyama vya upinza yanatekelezwa na serikali ya Dr magufuli.


Wakizungumza katika mkutano na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa kadi za ccm makada hao wa chadema wamekanusha kuhusu suala la kununuliwa kama ambavyo linazungumzwa na wapinzani zadi ya kulidhishwa na mwenendo wa kiutendaji wa serikali Iliyopo madarakani.

Kwa upande wake katiku wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike na Erasto Ngole ambae ni katibu mwenezi mkoani humo wanasema jamii za watu wanjombe zitegemeee kuona makada wengi wa upinzani wakijiunga na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama hicho kimejipambanua kuwapigania watanzania.

Viongozi wengine waliokuwepo katika Mkutano huo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Antony Katani,Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe Angela Mwangeni,Katimu wa Hamasa na Chipukizi mkoa Johnson Mgimba,Katibu mwenezi wilaya ya Njombe Hitra.

 Matukio yote Tazama Picha Hizi hapa Chini.




















































































































Hakuna maoni: