Dstv Tanzania

CCM MKOA WA NJOMBE YA UNGANA NA VIJANA KATIKA MICHEZO




Chama cha mapindzuzi Mkoa wa Njombe chajiwekeza katika vijana ili kuweza kukidhi mahitaji yao pale wanapoomba.


Kimeandaa ligi nyingine ya mpira wa miguu kata ya ramadhani, iliyoombwa na vijana wa kata ya  Ramadhani, ligi hiyo itahusisha vijiji tisa vinavyounda  kata ya ramadhani.


Ligi hiyo imedhaminiwa na viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya ya Njombe, wadhamini wa ligi hiyo ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Erasto Ngole, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Nehemia Tweve, katibu wa UVCCM Wilaya ya Njombe Daniel Mhaza na Katibu wa Siasa na Uenezi kata ya Ramadhani Michael Msigwa.


Ligi hiyo itazinduliwa leo  tarehe 29/09/2018 saa 9:30 alasiri katika uwanja uliopo Kibena shule ya Msingi. 

Mgeni rasmi wa kuzindua ligi hiyo ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.


Viongozi wa CCM kata ya ramadhani unawaarika wananchi wote wa Njombe kushiriki uzinduzi huo wa ligi, uzinduzi huo  utaambatana na maandamano toka kibena Hospitali.


Asante

Na Erasto Kidzumbe
0753580894

Hakuna maoni: