Dstv Tanzania

DIWANI WA CHADEMA KATA YA MJI MWEMA MJINI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE NOLASKO MLOWE ATIMUKIA CCM

Na Elizabeth John,Njombe.


Diwani wa kata ya Mji Mwema Mjini Makambako Mkoani Njombe Nolasko Mlowe,ambaye pia ni mwenyekiti wa jimbo la Makambako Chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA amekihama chama hicho Leo na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM kwa kuunga mkono jitihada za rais John Pombe Magufuli.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisi za Chama cha mapinduzi CCM kata ya mji mwema mjini Makambako,Mlowe amesema ameamua kujiunga na CCM na kwamba anaamini anakwenda kutatua kero zote za wananchi kutokana na kwamba ccm ina ilani na mikakati inayotekelezeka.


"Nilivyokua Chadema nilikua ntashindwa kutatua changamoto za wananchi vile inavyotakiwa kwani hakuna ilani wala mkakati ambao unaeleza tunatakiwa tufanye nini kwa wakati gani...na sasa nimeamua kuja ccm kwa sababu wanasera na taratibu zinazoeleweka"amesema Mlowe.


Naye Katibu wa chama cha mapinduzi Ccm wilaya ya Njombe Anton Katani amesema kwamba chadema wameshashindwa kujijenga hoja zenye mashiko na ndio maana wanachama na viongozi wanakihama chama hicho.


Mwisho.

Hakuna maoni: